Habari

Hizi ni nchi 6 Afrika ambazo marais wake wa sasa ni watoto wa marais waliopita

Suala la mtoto wa rais kuja kugombea urais lilionekena kama tatizo na linaendelea kuonekana kama tatizo barani Afrika lakini mambo si kama hivyo wanavyodhani waafrika wengi.

nyerere_karume_and_moyo

Mwezi uliopita, waziri mkuu wa Canada ambaye ni mtoto wa Justin Trudeau aliyekuwa waziri mkuu wa 15, alichaguliwa kuongoza serikali ya nchi hiyo.

Ingawa hali hiyo si ya kawaida kwenye nchi nyingi duniani, hali hiyo hiyo iliweza kushuhudiwa nchini Marekani pale ambapo Rais wa awamu ya sita John Quincy Adams alichaguliwa kuiongoza Marekani wakati baba yake ndiye aliyekuwa Raisi wa awamu ya pili John Adams.

Hali hiyo hiyo ilijirudia tena kwa Rais wa awamu ya 43 George W. Bush aliyeongoza vipindi viwili akiwa ni mtoto wa Rais wa Marekani wa awamu ya 41 aliyeongoza kipindi kimoja tu.

Ukienda barani Asia utakuta baba anamwachia binti yake kuongoza nchi kama binti wa aliyekuwa Rais wa Korea ya Kusini, Park Chung-hee aliyemwachia Pak Geu-hye ambaye ni Rais wa sasa wa Korea ya Kusini aliyechaguliwa kwa uchaguzi wa demokrasia kabisa na kuwa mwanamke wa kwanza kuingoza nchi hiyo.

Tukirudi barani Afrika tunakutana na hali hiyo hiyo kwa baadhi ya nchi kama Zanzibar, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Botswana, Gabon na Togo.

Zanzibar

Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alipata wadhifa huo baada ya kutokea mapinduzi yaliyosababisha kupinduliwa kwa Sultani wa mwisho wa Sultan Jamshid bin Abdullah January 1964.
Miezi mitatu baadaye, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa na Karume akawa makamu wa kwanza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Mwalimu Julius Nyerere akiwa Rais.

Jina la Karume lilirejea tena baada ya Amani Abeid, mtoto wa Karume kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na kuingia madarakani November 8, 2000 hadi November 3, 2010.

Togo

Faure Essozimna Gnassingbe ambaye ni rais wa sasa nchini Togo alishika wadhifa wa urais baada ya kufariki baba yake Marehemu Gnassingbé Eyadéma mwaka 2005. Jumuiya za kimataifa zilipinga wadhifa huo wa kumtangaza kuwa rais wa nchi hiyo hivyo Togo ililazimika kuitisha uchaguzi wa kidemokrasia mwaka 2009 ambapo alishinda na kuiongoza rasmi nchi ya Togo kama rais halali wa nchi hiyo.

Mwaka huu ameshinda tena uchaguzi hivyo ataiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine kwa miaka mitano zaidi.

Togo-1024x572

Gabon

Ali Bongo Ondimba, ni mtoto wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Omar Bongo ambaye aliiongoza Gabon tangu mwaka 1967 mpaka alipofariki 2009.

Baada ya kufariki Mzee Omar Bongo mwanae Ali Bongo Ondimba aligombea nafasi ya Urais kupitia chama cha Gabonese Democratic Party mwaka 2009 ambapo alishinda kwa kura zilizobeba asilimia 42% ya kura zote.
Ali Bongo hana tofauti na baba yake kwani ilipofika mwaka 2010 alituhumiwa kwa kutumia fedha za walipa kodi wananchi wake na kujinunulia jumba la kifahari nchini Ufaransa.

Gabon-1024x434

DR Congo

Joseph Kabila, ambaye ndiye Rais wa sasa kuanzia mwaka 2001, alishika ofisi hiyo siku 10 baada ya kuuawa kwa Baba yake Marehemu Laurent-Désiré Kabila. Vile vile alichaguliwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2006 na kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili mwaka 2011. Kabila aliyezaliwa miaka ya 1970 ameongoza Congo kwa miaka 18 hadi sasa.

DRC-1024x377

Kenya

Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Kenya ambaye ni mtoto wa muasisi wa taifa hilo marehemu Jomo Kenyatta. Uhuru Kenyatta anayejulikana kwamba ndiye rais mwenye umri mdogo aliyewahi kuitawala Kenya, aliingia madarakani mwaka 2013. Rais Kenyatta amesafiri nje ya Kenya mara nyingi zaidi akimzidi baba yake ambaye aliweza kusafiri mara mbili tu kwenda nje ya Kenya kwa miaka 15 ya utawala wake.

Kenya-1024x416

Botswana

Luteni Ian Khama, rais wa sasa wa nchi hiyo ni mtoto wa wa rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Seretse Khama. Kutokana na Historia, familia hii inatoka ukoo wa kifalme wa mzee Sekgoma II na Malkia Tebogo. Ian alizaliwa tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 1953 wakati wazazi wake wakiwa kizuizini huko Uingereza.

Alishika madaraka ya kuiongoza nchi hiyo mwaka 2008 na vile vile alifanikiwa kupewa kuongoza miaka mitano ya kwanza baada ya kushinda uchaguzi wa wabunge na vile vile mwaka 2014 aligombea na kushinda tena.

Botswana-1024x529

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents