BurudaniVideos

Hizi ni nyimbo 5 zilizorudia nyimbo za zamani na kuhit tena

Diamond Platnumz na Raymond (Ray Vanny) wameurudia wimbo maarufu wa Saida Karoli, Salome na kuuweka katika mahadhi ya kisasa zaidi huku pia wakiipata video kali.

Salome ndio ulikuwa wimbo uliomfungulia njia Saida Karoli na kumfanya awe mwanamuziki aliyeingiza fedha nyingi enzi zake. Kama yeye hakuingiza fedha nyingi, basi uongozi wake ulifaidika kwa kiasi kikubwa.

Hakuna shaka Salome version ya Diamond na Ray itahit.

Katika muziki, kurudia nyimbo zilizoimbwa na wasanii wengine, ni kitu cha kawaida. Katika nchi zilizoendelea hiki kinafanyika kila leo. Na kwa wasanii waliotumia process halali, huwafaidisha waimbaji wa mwanzo kwa kuwalipa gharama kadhaa.

Japokuwa kwa Tanzania mtindo huu si maarufu sana, huko nyuma kumewahi kufanyika nyimbo zilizorudia nyimbo za mwanzo na kufanya vizuri sana.

Hizi ni nyimbo 5 miongoni mwa zile zilizofanya vizuri.

1.Ray C Mahaba ya Dhati – Original by Nasma Hamis

Mahaba ya Dhati awali uliimbwa na malkia wa zamani wa muziki wa Taarab, marehemu, Nasma Hamis. Baadaye Rehema Chalamila aka Ray C alikuja kuurudia na ukafanya vizuri sana.

https://www.youtube.com/watch?v=c_y-UAuC2TI

2. Msafiri – Kwanza Unit – (Original Mimi Msafiri by Orchestra Safari Sound)

Katika nyimbo ambazo kundi la Kwanza Unit lilizitoa na ukafanya vizuri basi ni Msafiri. Kundi hilo ndio linafahamika miongoni mwa waasisi wa hip hop ya Tanzania.

Kwanza Unit waliuweka wimbo huu wa Orchestra Safari Sound katika mahadhi ya hip hop na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

3. Muhogo wa Jang’ombe – Lady Jaydee (Original by Bi. Kidude)

https://www.youtube.com/watch?v=sZvZksszNW0

Kiukweli mimi ni mmoja wa watu ambao hawakuwa wakiujua wimbo original wa Bi. Kidude. Nilikuja kuujua baada ya kusikiliza version ya Lady Jaydee iliyopikwa kiustadi na kuupa uhai tena wimbo huu uliotungwa na mwanamuziki hodari wa Taarab kuwahi kutokea Tanzania, marehemu Bi. Kidude.

4. Fina Mango – Shoga (Original by Vijana Jazz)

Naamini kuna wengi ambao hawajui kuwa pamoja na kuwa mtangazaji hodari wa redio, Fina Mango ni muimbaji mzuri na aliwahi kutoa album yake iliyokuwa na wimbo ‘Shoga’ ambao awali uliimbwa na Vijana Jazz Band.

5.Mwana FA f/ Linah – Yalaiti (Original by Bi. Kidude

Mwana FA ni shabiki mkubwa wa muziki wa zamani hususan taarab asilia kutoka mwambao. Hiyo ilimpelekea aungane na Marco Chali kufanya version ya rap ya wimbo wa Bi. Kidude, Yalaiti. Linah alizitendea vyema sauti za Bi. Kidude kwenye chorus ya wimbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents