Burudani

Hizi ni sababu 5 za kwanini ni ngumu kuwa sawa kimuziki na Nigeria

Nigeria imekuwa ikitupiga bao kwa mambo mengi tangu kitambo. Miaka ya nyuma, Nigeria ilikuwa ni nchi iliyosifika mno kwenye soka barani Afrika. Wachezaji wengi wa Afrika walioanza kuvichezea vilabu vya Ulaya kwenye soko la kulipwa walianza kutokea Nigeria.

page

Baada ya nchi kama Cameron, Ivory Coast, Ghana na zingine kuwa na wachezaji pia kwenye vilabu hivyo, hilo likawa jambo la kawaida.

Lakini katika kipindi cha miaka 10 hadi sasa, Nigeria ikaja kuibuka kama ‘super power’ si tu kiuchumi barani Afrika, bali pia katika muziki.

Nigeria imetengeneza kiwanda cha muziki imara na kikubwa kuliko nchi yoyote Afrika, ikiwemo Afrika Kusini ambayo pamoja na kuwa ni kitovu cha muziki wa Afrika.

Ukiambiwa kutaja orodha ya wasanii 20 wa Afrika wanaofanya vizuri, asilimia 70 ya wasanii hao inaweza kutawaliwa na Wanaijeria. 2 Face, D’Banj, P-Square, Flavour, Wizkid, Davido, Iyanya, Tiwa Savage, Burna Boy, Ice Prince, Olamide kutaja wachache tu.

Muziki wa Nigeria unahit kila kona ya bara la Afrika. Si ajabu kuhudhuria harusi hapa Tanzania na kubaini kuwa asilimia 80 ya nyimbo zinazochezwa ni za wasanii wa Nigeria. Ukienda club, ukitoa muziki wa Marekani, ni muziki wa Nigeria ndio unaochezwa zaidi kuliko hata Bongo Flava.

Hata Ghana, jirani zao nao wanalia kwakuwa muziki wa Nigeria unachezwa zaidi nchini mwao kuliko za wasanii wao wenyewe.

“A DJ can play 10 Nigerian songs and cut in with just a song from Ghana. This should not be tolerated in Ghana. I’m against banning of Nigerian or foreign songs in Ghana but the fact that Ghana songs play second fiddle to these foreign songs right here in Ghana is not right,” ilisema makala moja kwenye mtandao wa Graphic.com.

Hata Cameroon pia, mambo ni yale yale. Makala iliyoandikwa kwenye mtandao wa PR Gorreti isemayo ‘The invasion of Nigerian music over Cameroon radio airwaves’ imeongelea jinsi muziki wa Nigeria unavyochezwa zaidi nchini humo.

“From the music played at weddings to those blazing out of discotheques and shops; ninety percent of the time, it was Nigerian music,” imesema makala hiyo.

Wakati ambapo tunajitahidi kwa nguvu zote kuwa kama wao, kuna mambo kadhaa ya kuzingatia ili kujua kwanini muziki wao umefanikiwa kiasi hicho. Haya ni mambo matano niliyogundua:

1. Wanaijeria wanapenda na kuuthamini muziki wao

Wakati ambapo tunashangaa kuona muziki mwingi unaochezwa kwenye mahafali ya shule zetu ni wa wanaijeria, kwao hali ni tofauti kabisa. Wanaijeria ni wao na muziki wao. Hawataki kusikia muziki wa Tanzania, Kenya wala Uganda.

Ni wasanii wachache sana kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki wanaofanikiwa kusikika kwenye vituo vya redio vya Nigeria. Wanahesabika kabisa – Diamond, Vanessa Mdee, AY, Victoria Kimani na Sauti Sol, kwisha kazi!

Asilimia zaidi ya 70 ya nyimbo zinazochezwa nchini humo ni nyimbo za Nigeria. Nenda club, nenda kwenye harusi, nenda kwenye sherehe yoyote ile, utasikia wakicheza muziki wao zaidi. Kwahiyo kiwanda chao kinajitosheleza chenyewe, tofauti na sisi.

2. Kiwanda cha muziki Nigeria ni kikubwa zaidi kuliko nchi zingine barani Afrika

Kiwanda cha muziki nchini Nigeria kinakadiriwa kufikia thamani ya dola bilioni moja ifikapo mwaka 2016. Takwimu zinaonesha kuwa mapato ya show za muziki za wanaijeria yamefikia dola milioni 105 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Obi Asika, CEO wa Storm Records, moja ya kampuni za record label kubwa nchini Nigeria, makampuni ya simu yaliingiza dola milioni 150 kwa kuuza nyimbo kwenye miito ya simu na huduma zingine mwaka 2011.

3. Kuna record label za uhakika

Nigeria ndio nchi yenye record labels nyingi na za uhakika kuliko nchi nyingine barani Afrika. Kama zilivyo record label za Marekani, makampuni haya humsimamia msanii na kugharamikia gharama zingine zote za kumtangaza.

Miongoni mwa record label hizo ni pamoja na Empire Mates Entertainment iliyomtoa Wizkid na inayomilikiwa na Banky W, Mavin Records yenye wasanii kama Dr SID, Tiwa Savage, D’Prince, Di’Ja na wengine, Mo’Hits Records yenye wasanii kama D’banj na Wande Coal.

Zingine ni Chocolate City yenye wasanii kama M.I, Ice Prince, Victoria Kimani na wengine, 960 Music Group inayomsimamia 2face Idibia na zingine.

4.Makampuni yanawapa endorsement kubwa wasanii

Wasanii wa Nigeria ndio wanaongoza barani Afrika kwa kuwa na mikataba minono ya matangazo na makampuni ya biashara. D’Banj ni msanii anayeongoza kwa kuwa na mikataba mingi zaidi ikiwa ni pamoja na mkataba na kinywaji cha Power Fist, Bank of Industry (BOI), Globacom, Beats by Dre na Ciroc Nigeria.

P-Square wana mkataba wa miaka mingi na kampuni ya simu ya Glo huku mwaka jana Peter Okoye akisaini mkataba wake peke yake na Olympic Milk.

Banky W ana mkataba na Samsung na Ciroc Nigeria huku Tiwa Savage akiwa na mkataba na MTN, Forte Oil, Pepsi, Maggi na Konga. Wizkid ana mkataba na Pepsi, MTN Nigeria na Guinness Nigeria huku Davido akiwa na mkataba na MTN Nigeria, Guinness Nigeria na Close Up.

Kwa upande wa Iyanya ana mkataba na MTN wenye thamani ya Naira milioni 60m, mkataba wa $350,000 na kampuni ya kompyuta ya Zinox na mwingine wa naira milioni 35 na kampuni ya utengenezaji simu ya Solo Mobile.

Ice Prince na Olamide wana mkataba wa ubalozi na kampuni ya Etisalat Nigeria wenye thamani ya Naira milioni 20 kila mmoja.

5. TV za kimataifa zimetawaliwa na Wanaijeria

Angalia Channel O, Trace TV na MTV Base, utagundua kuwa nyimbo nyingi zinazochezwa ni za wasanii wa Nigeria. TV hizo zinaitegemea zaidi Nigeria kama kiwanda kikubwa zaidi kinachowapatia content ya kurusha hewani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents