Habari

Hizi ni sababu za kwanini wanawake huendelea kukaa kwenye uhusiano wenye mateso

Nimekuwa nikisoma makala mbalimbali na kutambua ya kuwa wanawake wengi huendelea kuvumilia ukatili wa waume wao au wapenzi wao kutokana na sababu mbalimbali ambazo wengine wetu tulio nje hatuwezi kuzijua kwa undani wake hasa. Lakini kuna sababu za jumla ambazo zimewafanya kuendelea kuvumilia mateso hayo au hali hiyo kama ifuatavyo;

Utokeaji wa matukio hayo na madhara yake

  • Wengi hufanyiwa ukatili si kwa muda mrefu, inamaanisha inatokea mara chache chache
  • Wengine huambiwa “Nisamehe mpenzi wangu, sitorudia tena” hivyo kuamini maneno hayo na kuendelea kukaa
  • Kwa ujumla, ukatili wenye madhaea kidogo na haujitokezi mara kwa mara hivyo kumhamasisha kuendelea kukaa kwa kuamini kwamba ni maisha na hakuna mtu ambaye hapitiii matatizo kama hayo.

Maisha ya Utotoni

  • Wanawake wengine huendelea kuvumilia hali ya ukatili kutokana na mazingira waliyokulia ambayo kulikuwa na ukatili pia hivyo wameweza kukubaliana nayo kwa kupenda au kutokupenda.
  • Namna ambavyo aliweza kunyanyashwa na kufanyiwa ukatili wakati akiwa mdogo na kama ni majeraha ya mwili au hisia n.k) vivyo hivyo anaweza kuendelea kukaaa na mtu huyo.

Wanawake wengi wana uchumi tegemezi

  • Kama mwanamke kiuchumi anategemea kwa huyo jamaa kila kitu anakuwa hakuna njia nyingine. Kwa mtizamo wake ni bora avumilie mateso ili apate hifadhi ya maisha kiuchumi.
  • Hali ya uchumi wa sasa pamoja na watoto, hivyo utakuta wanawake wengi hawana ujuzi wa soko.
  • Woga

    • Wanawake wengi wanaamini au kuchukulia wanaume wao kama Miungu, hivyo wanashindwa kuona njia yoyote ya kujilinda. Uoga alionao anaona ni haki kabisa na anaishi nao.
    • Kama akitoa taarifa polisi au majirani wakatoa taarifa polisi anaona atapata hali ngumu zaidi hivyo anaamua kunyamaza tu.
    • Anaaamini hana nguvu ya kubadilisha mambo.

    Imani kuhusu Ndoa

    • Dini na imani za tamaduni na kimila inamlazimu aonyeshe kuwa ndoa ni nzuri hata kama anaumia huko ndani.
    • Wengine wameendelea kukaa kwenye ndoa zenye mateso kwasababu ya watoto.
    • Wengine wanaamini mateso ndani ya ndoa au mahusiano ni sehemu katika ndoa hiyo.
    • Wanawake wengine wanaamini umuhimu wa mahusiano mazuri au ndoa nzuri ni jukumu lake binafsi na si la mwanamme pia kuhakikisha ndoa inakuwa ya amani au mahusiano yanakuwa ya amani.

    Anaamini nini kuhusu Wanaume?

    • Bado anampenda na hisia zake bado zibo huko.
    • Anaamini kwamba wanaume wana nguvu na atampata popote atakapo kwenda. Hivyo imani na woga wake unatokana na mambo yanayoendelea, hivyo mwanaume hawezekani.

    Kwa huruma na ujinga mwingi hudhani huyo ndio pekee atakayeweze kumhurumia na kubadilika.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents