Habari

Hizi ni simu zitakazokosa huduma ya Whatsapp

Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.

12938129_1170936479591682_5286111390182098593_n

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”

WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016. Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.

Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.

160212101736_blackberry_phone_624x351_reuters

Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
Android 2.1 and Android 2.2

Blackberry OS 7 and earlier

Blackberry 10

Nokia S40

Nokia Symbian S60

Windows Phone 7.1

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.”

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents