Hong Kong ndio mji aghali zaidi duniani, waupiku mji wa Luanda
Mji wa Hong Kong umekuwa mji aghali zaidi duniani baada ya kuupiku mji wa Luanda, Angola. Hii ni kulingana na wafanyakazi wa kimataifa katika utafiti wa kila mwaka unaofanywa na shirika la Mercer.
Hong Kong
Mji wa Luanda una utajiri mkubwa wa mafuta
Luanda uliokuwa unaongoza orodha hiyo kwa miaka mitatu mfululizo kwa sababu za gharama za kodi, bidhaa za kigeni na usalama wa utajiri wa mafuta lakini kwa sasa umeshuka kufuatia kudhoofika kwa sarafu yake.
Zurich
Singapore
Mji wa Zurich ni wa tatu Singapore ni ya nne. Hizo ni nafasi katika orodha hiyo ambazo hazijabadilika kwa mwaka mmoja sasa. Mji wa Tokyo sasa umepanda hadi nafasi ya tano.
Miji 5 aghali mwaka 2016
1. Hong Kong
2. Luanda,Angola
3. Zurich, Switzerland
4. Singapore
5. Tokyo, Japan