Habari

Hongera Mwana FA na Lady Jaydee kwa kuandika historia June 14

June 14, itakumbukwa daima kwa jinsi muziki wa Tanzania ulivyoandika historia kutokana na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa show mbili pinzani, The Finest ya Mwana FA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya taifa na Miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee iliyofanyika Nyumbani Lounge.

page

Bongo5 ilikuwepo kwenye show zote mbili kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho hivyo naongea kwa kujiamini kuwa show zote mbili zilifanikiwa sanaaaaaaaa sababu tuliona kwa macho yetu wenyewe.

Kwa wale waliooenda kwenye show ya Lady Jaydee watakubaliana nasi kuwa barabara zote za jirani na Nyumbani Lounge zilifunga kutoka na kujazana kwa misururu mirefu ya magari iliyokuwa ikielekea hapo. Mistari mirefu ya mashabiki waliokuwa na tiketi zao iliyofika hadi Best Bite ilionekana wazi. Lady Jaydee alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuvuta umati wa aina yake kwenye show hiyo na bahati mbaya wengine kukosa tiketi. “Nimetamani kulia, manake watu wengine wameshindwa kuingia kabisa wamerudia barabarani. Ila tunashukuru kwa yote,” ametweet.

DSC_4453

Akisindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Profesa Jay, Sugu, Juma Nature, Grace Matata na wengine, Lady Jaydee alizikonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa mara ya kwanza Lady Jaydee alionekana kwenye mavazi ya aina yake kama yanayotumiwa na waendesha magari ya mashindano. Kwa Lady Jaydee siku ya jana ni wazi hatoisahau katika maisha yake. “Nashindwa kulala kabisa, nina furaha kupita kiasi…. Asanteni kwa yaliotokea jana,” ameandika Jide.

Pamoja na fedha ya kiingilio, jana Lady Jaydee alituzwa fedha nyingi jukwaani kutoka kwa mashabiki walioguswa na nyimbo zake. “Watanzania nawapendeaga zaidi pale kwenye kautaratibu ketu ka kutunzana hela jukwaani, jana mmeniogesha,” ametweet Jide.

Kwa upande wa Mwana FA, mambo yalikuwa yale yale, ni furaha. Show yake ilifanikiwa mno, tofauti kabisa na imani ya baadhi ya watu kuwa show yake haikwenda vizuri. Show yake ilikuwa na tiketi 400 tu na zote zilinunuliwa. Ukumbi mzima ulikuwa ukiinuka mara kwa mara kuimba na kumshangilia Mwana FA aliyekuwa amevaa suti ama shati na suspender mwanzo hadi mwisho wa show.

IMG_5543 (533x800)

Mwana FA alipewa shavu na wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Ben Pol, Man Dojo na Domo Kaya, Maua Sama pamoja na Dully Sykes. Kama Lady Jaydee, Mwana FA naye hatoisahau siku ya jana.

Mashabiki wanapaswa kufahamu kuwa show ya Lady Jaydee na Mwana FA hazikuwa kwaajili ya kushindana wao kwa wao ama kuoneshana nani anaweza na mwenye mashabiki zaidi. Zilikuwa ni show za kujipatia mkate wao kwakuwa muziki ndio kazi yao.

Usiku wa jana umeshuhudia mashabiki wakienda ‘bila kushurutishwa’ kwenye show waliyopenda wenyewe. Aliyeenda kwa Jaydee amerudi nyumbani na furaha na aliyeenda kwa Mwana FA amerudi kwa furaha. Mwisho wa siku mashabiki wa Mwana FA na mashabiki wa Lady Jaydee wote ni kaka na dada wa Tanzania. Kila msanii apewe pongezi zake anazostahili kwa kazi nzuri aliyoifanya jana bila kutawaliwa na hisia za kishabiki zaidi.

“Hongera kwa kamando Jide kwa kutimiza miaka 13 ya mziki. Wewe ni legend, malkia wa mziki wa kizazi kipya. Hongera pia kwa show nzuri jana. Hongera pia MwanaFa kwa kupiga hip hop live ukishirikiana na bendi ya Njenje. Mziki Tanzania unapiga hatua. Mapambano yaendelee,” ameandika Jokate Mwegelo.

Tunawapongeza Lady Jaydee na Mwana FA kwa kazi na maandalizi mazuri ya show zao.

Kukupa mfano wa jinsi show za wasanii hawa zilivyofanikiwa, hizi ni baadhi ya pongezi kwa kila mmoja.

MWANA FA

Kelvin J Twissa ‏

Today at The Finest I Witnessed the Rebirth of Hip Hop in Bongo. Bongo Flava was reborn and this shall be televised.

Obrien Koola ‏

#TheFinest was the best show in town hate it or love it @MwanaFA thanks for the best show bro. Hope to see more of you in your next show.

KiBeIbY MoMo

#TheFinest ilikua best show ever seen to me @MwanaFA is the best No Homo,hata waseme wasemalo deep in my Heart your the Best….YOLO.

Mwamvita Makamba

Massive congratulations to my brother @MwanaFA for a fabulous show last night ! You set the trend for a class! You looked super fly maaan.

Abdallah Singano

I think #TheFinest should have been priced at 100k, coz we paid far less than what we got

Dina Marios

Am So pround of you @MwanaFA jana uliipeleka hip hop ya bongo level za mbele na live band na wananjenje.Hiyo ni big step kwa career yako.

Mahmud A Kullane

It’s been awhile since ive attended any concert of any sort but it was worth the wait #TheFinest was a spectacle, Heshima yako.

kheri kheri

@MwanaFA ,nw that’s what’s called #Classic..great show,classy outfits…Tisha sana…Proud sana of ya Uncle..#No Regrets.

POWER MABULA ‏@IamNchaKALIH

@MwanaFA nakushukuru wewe, wana njenje pamoja na wadhamini wako kwa kuuwakilisha HIP HOP in a new way?! You killed it bro.

LADY JAYDEE

Profesa Jay

ASANTENI sana Watanzania kwa KUFANIKISHA salama Miaka 13 ya lady jay dee MBARIKIWE sana maana hatuwezi kufanya lolote bila Nyinyi…BLESS!!!

Sugu

Mission accomplished last nite : now at the airport leaving Dar S salaam back to Mbeya…

Rama Dee

Watu waliofika kwenye shoo ya @JideJaydee ni watu wenye upendo katika hii Sanaa.. nasikia poa kazi imemalizika salama. Kazi nzuri sana…natumaini huu ni mwanzo kazi ndio inaanza sasa…

Haji Mapowder

Lady jay dee, sisi mashabiki tumejitokeza kwa wing ktk show yko kuonesha kuwa ? liliopangwa na Mungu?? Binadamu hawez Pangua,siku zote usimpe Binadamu cheo cha mungu wko.

Sheila Cleveland Nkata

Jamani mlimuona dada alivyochana ile part ya mr blue kwa mliokuepooo yani noumaaa mijusi woteee sahz wamejitupa kwenye vyoo vya shimoo….chezea anaconda.

Aweso Hammie

I do appreciate you ccta!!!keep doing what you do..n let them know that they can’t take what you were gifted by almighty GOD! 1 lov.

Innocent Mathew

Dada unaonaje siku ukiandaa moja ingine kama ile uwanja wa taifa patajaa maana jana ilikua qwii qwii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents