HabariUncategorized

Hospitali ya Mama na Mtoto iliyojengwa kwa bilioni 9 kwa jitihada za RC Makonda yazinduliwa (Video)

Rais wa Shirika la Misaada la Korea Kusini Koica Bi.Lee Mi Kyung amezindua hospitali ya Mama na Mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitiada binafsi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alietafuta wafadhili hao.

Ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa umegarimu zaidi shillingi billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya upasuaji, vyumba vya madaktari, maabara,chumba cha mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti, Theater, vyumba vya kujifungulia, ICU, Vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za Familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna kila kitu.

RC Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga hospitali hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.

Aidha RC Makonda amemuomba Rais wa KOICA kumjengea Hospital nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshukuru serikali ya Korea kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.

kwa upande wake Rais wa KOICA Bi. Lee Mi Kyung amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha amani tofauti na Mataifa mengine.

Uzinduzi wa Hospital hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya wagonjwa (ambulance).

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents