Habari

Hospitali ya Morogoro yathibitisha zaidi ya watu 59 wamefariki dunia, baada ya lori la mafuta kulipuka – Video

Hospitali ya Morogoro yathibitisha zaidi ya watu 59 wamefariki dunia, baada ya lori la mafuta kulipuka

Lori la mafuta limelipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogogoro, Mashariki mwa Tanzania nzaidi ya watu 50 wawethibitishwa kufariki dunia katika ajali hiyo. Gazeti la Mwananchi linamnukuu kamanda wa Polisi wa Morogoro Wilbroad Mtafungwa akithibitisha vifo vya watu 57 mpaka sasa.

Inahofiwa kuna miili mingine ambayo imebanwa chini ya lori hilo baada ya moto kulipuka.

Bado mamlaka husika hazijathibitisha chanzo cha ajali hiyo, lakini inadaiwa wengi wa waliopoteza uhai walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema waendesha piki piki ndio walioathirika zaidi na mkasa huo.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Rita Lyamuya amethibitisha kupokea majeruhi 60 58 wakiwa wanaume na wawili wananwake lakini pia kupokea miili ya watu 60.

Mji wa Morogoro ni moja ya njia kuu za malori yanayobeba shehena ya mizigo na mafuta kutoka bandari ya Dar es Salaam.

Bado haijafahamika lori hilo lilikuwa linamilikiwa na kampuni gani ya usafirishaji na iwapo lilikuwa linaenda nje ya Tanzania ama la.

Baadhi ya watu wanatumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao na kuwapa pole Watanzania haswa wakaazi wa Morogoro waliohusika katika ajali hiyo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents