Michezo

Howard Webb astaafu kupuliza kipenga

Refa maarufu England na Mataifa ya Ulaya, Howard Webb amestaafu kuchezesha soka baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 25 na sasa atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya marefa (PGMOL).

1407328280598_wps_1_Referee_Howard_Webb_looks

Refa huyo mwenye heshima kubwa, amechezesha mechi zaidi ya 500 za Ligi Kuu ya England na nyingine za mashindano ya soka nchini humo tangu apande daraja mwaka 2003.

Webb pia amechezesha fainali mbili za Kombe la Dunia na mbili za Kombe la Mataifa ya Ulaya na kuweka rekodi ya kuwa refa wa kwanza kuchezesha fainali ya Euro na Kombe la Dunia kwa mwaka mmoja, 2010.

Webb alikuwa akishutumiwa sana kuibeba Manchester United.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents