Burudani

Huddah Manroe: I am not ‘HIV Positive’, atoa sababu za kupungua mwili kuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya!

Well, tumeyasikia mengi kuhusiana na mrembo huyu ambaye naweza kumuita (miss don’t care) sababu hajali chochote kinachosemwa juu yake, japo ni kati ya mastaa wanaozungumziwa sana katika mitandao kutokana controversial lifestyle yake. Na sasa amewajibu wale waliodhani ni muathirika.

huddah boss lady

Aliyekuwa muwakilishi wa Kenya katika BBA ‘The Chase’ Alhuda Njoroge a.k.a Huddah Manroe a.k.a The Boss Lady amekanusha uvumi ulioenea kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi kutokana na mabadiliko ya kupungua kwa mwili tofauti na alivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla Huddah ambaye alikuwa akihojiwa na Ghetto Radio amesema kilichosababisha mwili wake kupungua kwa kiasi hicho, ni matumizi ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine na madawa mengine makali aliyokuwa akitumia kipindi cha nyuma.

Huddah alisema kuna wakati katika maisha yake alikuwa amezungukwa na stress na kuamua kutumia madawa kwaajili ya kuzipunguza, kitu ambacho anakili kuwa sasa ameacha kabisa kutumia.

Manroe, amekuwa akiandikwa sana na mitandao toka achaguliwe kushiriki katika Big Brother Afrika mwaka huu (The Chase) ambayo kwa bahati mbaya safari yake ya mjengoni ilidumu kwa wiki moja tu na kutolewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents