Burudani

Huddah Manroe kuwasili nyumbani Kenya leo akitokea katika Big Brother ‘The Chase’

Aliyekuwa mwakilishi wa Kenya katika reality show ya Big Brother Africa “The Chase” inayoendelea, The boss lady Huddah Monroe anatarajiwa kutua nyumbani leo (June 5) baada ya kutolewa mchezoni jumapili iliyopita (June 2) ikiwa ni wiki moja tu toka shindano hilo lianze huko kwa mzee Madiba Africa Kusini.

huddah 22

Mrembo huyo toka aondolewe mchezoni amedhihirisha kuwa sasa amekuwa real star, ambaye ndani ya siku mbili ameshafanya interviews 42 kitu ambacho hakikuwahi kumtokea. Alitweet “42 Interviews in 2days….call me cursed or call me blessed…WHO is the STAR now???”

Huddah ni msichana mrembo ambaye ana maisha fulani ninayoweza kuyaita ya “utata”, na amejizoelea umaarufu mkubwa Kenya hasa kupitia mitandao ya kijamii kutokana na kuishi maisha ya kutojali watu wanavyomnyooshea vidole na kumsema vibaya.

Siku kadhaa toka atoke mjengoni Huddah amekuwa na kazi ya kujibu mashabiki wake twitter ambao kila mmoja alijibiwa jinsi alivyokuja, waliokuja kishari walijibiwa kishari na waliompongeza kwa kuwawakilisha walijibiwa vizuri.

Hizi ni baadhi ya tweet za Huddah kwa mashabiki wake:

-Seems like people expected me to have SEX on the first day in the house.Expectations lead to disappointments.Poleni saaana!

-Despite all the bullshit, I have a lot to be thankful for.

-I am happy i was evicted 1st nobody will ever forget this…and thats what fame is,staying in peoples minds…I am a legend in my own rights.

-7days in an enclosed enviroment is Eternity…if u think u could have done better,auditions happen every year.Good luck.

Kabla Huddah hajaondoka South Africa alipewa kifuta machozi kwa kufanyiwa shopping na big brother jana (June 4) na baadae kutweet akiwashukuru “@HUDDAHMONROE: Thanks @BigBroAfrica for taking me shopping today 😉 #RetailRelief! Dont tell”.

Huddah anategemewa kuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents