Burudani

Huddah Monroe awaonya wasichana wanaomuiga kuposti picha za nusu utupu mitandaoni

Msichana maarufu mitandaoni nchini Kenya, Huddah Monroe amewaonya wasichana wanaomuiga kwa kuposti picha za utupu mitandaoni.

Huddah

Huddah kupitia Snapchat amedai kuwa anafanya hivyo kwa sababu yeye analipwa kutangaza bidhaa za nguo za ndani (bikini) au Hoteli ambayo huwa amefikia kwa muda huo.

Najua wasichana wengi wananiangalia sana kama kioo cha jamii, lakini sidhani kama wengi wanavutiwa na picha zangu za utupu ninazotupia mitandaoni, Haya mambo inatakiwa wazazi wao na hao wenyewe waelewe kuwa mimi nalipwa kufanya hivyo kwa sababu ya matangazo ya bidhaa. Mara zote huwa nalipwa kutangaza bikini au hoteli ninayofikia, siwezi kufanya vile kujifurahisha,“ameandika Huddah.

Mrembo Huddah amejizolea umaarufu nchini Kenya kwa kuposti picha za nusu utupu mitandaoni, jambo ambalo limemfanya apate wafuasi lukuki mitandaoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents