Michezo

Huenda tukamuona Hazard akitua Manchester United,afunguka kuwa anahitaji kufanya kazi tena na Mourinho

Huenda tukamuona Hazard akitua Manchester United,afaunguka kuwa anahitaji kufanya kazi tena na Mourinho

Ikiwa ni likizo ya takribani wiki mbili kwa takribani ligi zote duniani kupisha michuano mbalimbali pia michezo ya kirafiki katika timu za taifa,kumeibuka sakata lingine linalomuhusu kocha wa Man United Mreno Jose Mourinho.

Kocha huyu amekumbwa na misukosuko mingi sana tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza zingine zikimuhusu yeye na wachezaji wake lakini zingine zikimuhusu yeye na viongozi wa timu hiyo.

Moja ya mgogoro uliopo katika klabu hiyo ni ule unaemuhusu yeye na kiungo wa klabu hiyo Mfaransa Paul Pogba,ambao wamekuwa hawana maelewano kwa muda sasa,mgogoro huo ukichangiwa na kile kinachosemekana mchezaji huyo kunyang’anywa usaidizi wa unahodha katika klabu hiyo baada ya kuongea maneno yanayohusishwa na kuuponda mfumo wa uchezeshaji wa Mreno huyo.

Sakata hilo likiendelea kunguruma katika klabu hiyo kubwa kabisa duniani,siku ya leo limeibuka lingine linalomhusu kocha huyo,ikiwa ni takribani miaka minne tangu kocha huyo kufukuzwa katika klabu ya Chelsea kwa kile kilichosemekana ni mgomo wa wachezaji wa timu hiyo kukumtaka kabisa Mreno huyo.

Moja ya wachezaji waliotajwa kuhusika katika mgomo huo ni pamoja na Mbelgiji anayekipiga katika klabu hiyo Eden Hazard ambaye amekuwa na msimu mzuri kabisa tangu msimu mpya uanze.

Mnamo tarehe 20 mwezi huu wa 10 kutafanyika matanange mkubwa sana kati ya Chelsea ambao watakuwa wenyeji kuikaribisha United katika mchezo wao wa ligi.

Hazard amefunguka kuwa “Anahitaji kufanya kazi tena na Mourinho” ameongea hayo wakati anazungumza na jarida la kimichezo la Ubelgiji linalojulikana kama HLN,Hazard ameuelezea msimu wa tatu wa Mourinho ndani ya United jinsi ulivyokuwa mbaya.

Hazard alisema “Ndani ya miaka yangu 12 ya soka nilikuwa na msimu mmoja mbaya, miezi sita iliyopita chini ya Mourinho, na ilikuwa ni kosa langu mwenyewe,” aliongeza. “Mara tu baada taji, tuliuliza Mourinho kama tunaweza kupata likizo ya ziada. Nikirudi ntakuwa vizuri.”  “msimu wa mwisho chini ya Mourinho hatukuufurahia, hatukushinda, tulikuwa na hali ya mbaya, tulifanya mazoezi bila furaha, ilikuwa ni nafasi nzuri kwa wapinzani kufanya vizuri,Kama ntaulizwa sasa hivi kocha ambaye ntaweza kufanya nae kazi lazima ntasema Mourinho Nilimtuma ujumbe wa kuomba samahani nilikuwa namhurumia sana, kwani Tulifanya kazi wote pia tulifurahia mafanikio yote pamoja”

Hazard amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka katika miamba hao wa London kujiunga na klabu ya Real Madrid kwa ndio matarajio yake ya muda wote,kwahiyo kupitia maneno hayo huenda tukamuona hazard akibadili uelekeo na kumfuata Mourinho kwa mara nyingine.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents