Michezo

Hujafanya tafiti, hunatakwimu funga mdomo – Haji Manara (Video)

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara hii leo amezungumza na waandishi wa habari na kuonyesha baadhi ya vipande vya michezo ambavyo hawakuridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na baadhi ya waamuzi wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Manara amewalalamikia waamuzi waliyochezesha michezo yao iliyopita dhidi ya Yanga SC ambayo anaaminikuliwa na Penati za wazi.

“Siku zote nikizungumza huzungumza bila takwimu, waingereza wanasema hujafanya tafiti, hunatakwimu huna haki ya kuzungumza funga mdomo wako sasa mimi siongei vitu kutoka hewani nimewaletea runinga ili muone matukio ambayo waamuzi wanavyochezesha dhidi yetu.”Amesema Manara.

Haji Manara ameongeza “Hebu tazameni Penati mbili za wazi za John Bocco muamuzi kaziacha hakutoa adhabu hakuna mtu aliyeandika wala wachambuzi waliyosema wao wanashikilia tu bilioni moja Kamusoko hayupo hizo apo waziwazi tumenyimwa.”

“Siamini kama yupo mtanzania anaweza kuleta ubishi kwenye ukweli ukiwa na tafiti wacha ushabiki muwamuzi yupo mbali unakuta anakwenda kutoa pasi hawa ndiyo waamuzi wa Bodi ya Ligi na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania sijui kesho watanifungia miaka 100 au milioni sijui.”

Kikosi cha Simba kinatarajia kusafiri tarehe 3 ya mwezi ujao kuelekea mkoani Mbeya kwaajili ya kujiwinda na Mbeya City mchezo wa duru la tisa la Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents