Habari

HUKUMU: Malkia wa meno ya Tembo atupwa jela miaka 17, mali zake zote zataifishwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu kifungo cha miaka 17 jela raia wa China, Yang Feng Glan maarufu kwa jina la ‘Malikia wa meno ya Tembo’, baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na  baishara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya TSh Bilioni 13.9 .

Yang Feng Glan

Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi baada ya kuwatia hatiani, washtakiwa hao.

Mbali na Malkia wa meno ya Tembo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 21/2014,  ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Mahakama pia imetaifisha nyumba na shamba la mshtakiwa  Malkia wa meno ya Tembo, iliyopo Muheza mkoani Tanga, ambavyo, vilihusika katika biashara ya meno ya tembo.

Hakimu Shaidi amedai kuwa katika shtaka la kwanza ambalo ni kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ambao ni ukusanyaji wa meno ya tembo 860, kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 15 jela.

Katika shtaka la pili, ambalo ni kushiriki, kusaidia, kukusanya na kusafirisha meno ya tembo 860 yenye uzito wa kilo 15,900, washtakiwa kwa pamoja watatumikia kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Hakimu Shaidi, amesema katika shtaka la tatu ambalo ni kujihusisha na ununuzi na kusafirisha meno hayo 860 sawa na tembo wazima 430, kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya TSh Bilioni 27.8 .

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 1, 2000 na Mei 22, 2014.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents