Burudani

Humphrey Polepole: Belle 9 na Bonge la Nyau wameshatoka hospitalini bado Lulu Diva

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole amehabarisha kuwa wasanii Bonge la Nyau, Lulu Diva na Belle 9 wameshatoka Hospitali na wanaendelea vizuri.

Wasanii hao walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze Alfajiri ya kuamkia siku ya Septemba 7, wakati wanarejea Dar Es Salaam baada ya kutoka kwenye kampeni za CCM, Kilolo Mkoani Iringa.

Akitoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, Humphrey Polepole ameandika kuwa,

Napenda kuwajulisha kuwa vijana wetu Belle 9, Bonge la Nyau wameshatoka hospitali na binti yetu Lulu Diva wote wanaendelea vizuri, Lulu Diva tunaomba Mungu atatoka hospitali leo, ahsante wote kwa support, ahsante zaidi Ummy Mwalimu, Muhimbili Taifa na Rais Magufuli, mungu awabariki

https://twitter.com/hpolepole/status/1303168454321672193

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents