Habari

Hussein Machozi kumshirikisha Wyre



Msanii wa Bongo Flava aliyehamia nchini Kenya, Hussein Machozi anatarajia kufanya ngoma na msanii wa zamani wa kundi la Necessary Noise, Wyre aka The Love Child.
Machozi amesema bado hajaupa jina wimbo huo na angependa mashabiki wake waupe jina wenyewe.
Kupitia Facebook jana ameandika:Okay, TANZANIA narudi nyumbani na wimbo mpya…HUSSEIN MACHOZI Ft. WYRE…wimbo bado haujapewa jina ila mtapewa nafasi ya kuchagua jina baada ya kuusikiliza wimbo ….pa 1.
Kutokana na mahojiano mafupi na Bongo5, Machozi amesema wimbo huo utafanyika kwenye studio ya Wyre iliyopo jijini Nairobi.
Akijibu swali ni wapi walikutana na Wyre na kupanga kufanya wimbo pamoja, Machozi amesema, “Tulikua kwa show moja hapa Nairobi tukaongea na kuamua kufanya.”
Ameongeza kuwa wimbo huo utahusu mapenzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents