BurudaniVideos

Hussein Machozi na Amba aliyetengeneza ‘Kwaajili Yako’ na ‘Utaipenda’ kufanya kazi tena

Miongoni mwa watayarishaji wa muziki wenye mchango mkubwa katika career ya Hussein Machozi ni Amba, anayefanyia kazi mkoani Iringa. Kipindi Machozi yupo chini ya usimamizi wa Tetemesha Records ya Kidboy, Amba alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu na label hiyo.

Kupitia utaratibu wake aliuanzisha hivi karibuni wa kujibu maswali 30 kupitia Instagram (@husseinmachozi100), Machozi amedai kuwa siku za usoni ni lazima atakuja tena kufanya kazi na Amba ambaye aliwahi kutengeneza midundo ya nyimbo zake ukiwemo Kwaajili Yako, Utaipenda aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na Full Shangwe aliyomshirikisha AY na DNA. Kidboy alikuwa mtayarishaji mkuu wa nyimbo hizo.

“Mimi naplan sana kufanya kazi na Amba sababu ni mtu ambaye anaipatia sauti yangu. Ni mtu ambaye anapiga beats ambazo mimi napita vizuri na ni mshikaji wangu tunaheshimiana sana,” amesema Machozi. “Nitaplan, lazima niende kufanya kazi Iringa kwa Amba. Nitakuwa kwenye management nyingine lakini sio lazima kazi zote ziwe zinatoka pale lazima tufanye huku na huku,” ameongeza.

Machozi ambaye kwa sasa yupo nchini Italia, amesema nyimbo atakazofanya na Amba atazijumuisha kwenye albamu yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents