Michezo

Hutaamini kiasi inacholipa NBC (Marekani) kuonesha Olimpiki na faida inayopata

Olimpiki ni michuano inayotumia fedha nyingi. Pamoja na nchi mwenyeji kutumia mamilioni ya dola kuandaa, fedha nyingi hulipwa na kampuni iliyochukua haki zote za kuyaonesha mashindano hayo kwenye runinga katika nchi husika.

Nbc-olympic-rings11

Kwa upande wa Marekani, kituo cha NBC ndicho kilichopata haki za kuonesha michuano hiyo tangu mwaka 1988. Mwaka 2011, NBC ilikubali kuilipa dola bilioni 4.38 kamati ya olimpiki kuonesha michezo hiyo hadi mwaka 2020, na kuwa mkataba wa gharama kubwa zaidi wa haki za runinga kwenye historia ya michezo hiyo.

May 7, 2014, NBC ilikubali kuufanya mkataba uwe wa dola bilioni 7.75 kwenda hadi michezo ya mwaka 2032.

Wanapata faida gani?

Kampuni ya NBCUniversal inatarajia kuingiza fedha nyingi zaidi kupitia olimpiki ya Rio licha ya kupungua kwa utamwaji wa mashindano hayo ukilinganisha na miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa data za Nielsen, wastani wa watu milioni 30.3 wameangalia vituo vya NBC pamoja na mtandaoni katika siku tano za mashindano hayo. Hiyo ni asilimia 8.6 pungufu za watazamaji wa NBC walioangalia michuano hiyo London mwaka 2012.

Hata hivyo NBC inatarajia kuingiza faida ya zaidi ya dola milioni 120 iliyoingiza kwenye michuano ya miaka minne iliyopita. Hadi sasa kampuni hiyo imepata matangazo ya dola bilioni 1.2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents