Burudani

Hutaamini rapper wa Marekani aliyetangaza kugombea Urais mwaka 2016!

Hillary Clinton ameshatangaza nia ya kugombea urais mwaka 2016 lakini huenda akakutana na upinzani kutoka kwa Mmarekani mweusi mwingine kama ilivyokuwa kwa Barack Obama mwaka 2008!

waka-flocka

Hata hivyo huyu si mshindani unayeweza kumdhania – ni rapper!

November mwaka 2012, Waka Flocka Flame alitweet: I’m dead ass running for president in 2016.” Na sasa amethibitisha kuwa hakuwa anatania.

Jumatatu hii, rapper huyo amezungumza na Rolling Stone kuelezea nia yake ya kuwa mgombea wa urais wa Marekani mwakani. Mgombea wake mwenza amemtaja kuwa ni DJ Whoo Kid.

Akiwa rais, Waka amesema jambo la kwanza atakalofanya ni kuhalalisha bangi!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents