Burudani

Hutaamini timu iliyopo nyuma ya Yamoto Band!

Yamoto Band imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi kifupi tu tangu ianzishwe.

10299835_347539675434983_2074124253_n

Ikiwa na takriban miaka miwili peke yake, bendi hiyo imetengeneza hits zaidi ya nne na kila siku imekuwa ikifanya show kwenye maeneo mbalimbali nchini. Nini siri ya mafanikio hayo? Ni timu iliyo nyuma yake.

Yamoto Band inasimamiwa na kwa ushirikiano wa Said Fela, Babu Tale, Diamond Platnumz, Mheshimiwa Temba na Chambuso.

“Diamond ni co-manager wa Yamoto Band,” Babu Tale aliiambia tovuti ya Mseto EA, Kenya.

“Wakati Yamoto inaanza yeye ndio alikuwa wa kwanza kusema kwamba ‘bosi hawa watoto watafika mbali, tuwatengenezee hiki.’ Kuna baadhi ya vitu Diamond ndio alitushauri. Mheshimiwa Temba ndio mkubwa wao wale madogo, mimi, Fela na Chambuso. Kwahiyo ni Diamond, Fela, Chambuso na mheshimiwa Temba ndio wanasimamia mafanikio ya wale madogo,” alisema Tale.

Katika hatua nyingine, Fela alisema kuna kitu kubwa Yamoto Band inakuja nacho mwaka huu.

“Hakijawahi kufanyika kwa msanii na management yake yoyote East Africa au Africa mpaka mwezi wa kumi wananchi watajua.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents