Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hutakosa tena furaha ukiona maisha ya Wakonta Kapunda na Ahmed Albaity

Kila nikiwaona Wakonta Kapunda na Ahmed Albaity naona hakuna sababu ya kutokuwa na furaha.

Furaha ni moja kati ya hazina kuu ambazo mwanadamu anatakiwa kutafuta,kutunza na kulinda kwa nguvu zake zote. Kimsingi hakuna sababu yoyote ya msingi inayoweza kuhalalisha mwanadamu kutokuwa na furaha ilimradi bado unavuta pumzi chini ya jua.

Bila shaka kama mtumiaji wa mitandao basi ni wazi utakuwa umeshawahi kuona picha moja ya binti mrembo ambaye baada ya ajali mbaya siku ya mahafali yake ya kidato cha sita alipooza sehemu ya mwili wake anaitwa Wakonta Kapunda. Mwingine ni kijana mtanashati aliyepoza vile vile baada ya kupata ajali akijaribu kuogelea anaitwa Ahmeid Albaity.

Wakonta Kapunda

Kama unawafuatilia utagundua kuna kitu kimoja kwao,muda wote wanatabasamu,muda wote wanaonyesha kuwa na furaha na muda wote wamejawa na maneno yenye matumaini!

Pengine wangelikuwa na sababu nyingi sana za kufanya muda wote kulia na kujawa na machungu lakini kwao kukosa kutembea na kufanya baadhi ya vitu hakujawafanya wakose furaha!

Kama maulana amekupa pumzi na huna furaha ni sawa na kumlaumu huyo aliyekupa pumzi kwamba kwanini anaendelea kukuweka hai,najua unaweza ukatafuta sababu elfu za wewe kutokua na furaha lakini ukikaa embu vuta taswira za wale vijana wawili waliokalia vitanda vyao miaka na miaka na bado hawajaruhusu hilo lichukue furaha zao? Walikuwa ndoto na malengo kama wengine ila imetokea ilivyotokea lakini furaha yao ipo pale pale.

Kimsingi furaha ni wewe kuamua kuwa na furaha na si vinginevyo, kila unapoamka asubuhi unakuwa na machaguo mawili kuwa na furaha au kutokua na furaha. Sasa kwanini unachagua kutokuwa na furaha eti kisa huna hiki,umeachwa,umetengwa,unaumwa? Ukijiona wewe una sababu za kuridhisha wakumbuke wakonta na Ahmeid!

Ahmeid Albaity

Acha kujilinganisha na wengine,kaa mbali na wanaokuletea machungu,amini furaha ndo utajiri mkuu kuliko utajiri wowote,epuka kuwekeza mambo moyoni na siku zote jipe matumaini kuwa Mungu anakuona na anajua haja zako pengine kuliko wewe. Kujisogeza machoni pake ni wewe kuonesha pamoja na yote una thamini pumzi aliyokuachia mpaka leo.

Kwa Wakonta Kapunda na Ahmeid Albaity,kuna mamia ya watanzania wenye shida na matatizo kama yenu. Kwa bahati nzuri nyie jamii inawafahamu kuonekana mkitabasamu pamoja na hali yenu mnawapa sababu za kuona kumbe inawezekana kuwa katika hali kama hiyo na bado nyuso zenu zikaendelea kugubikwa na tabasamu. You better keep that attitude alive mengine maulana anayajua.

Na Eliezer Gibson
Instargram: @gibson_elly

Sent from my iPhone

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW