Burudani

Huu ndio muda mzuri wa kuanza kazi – Enock Bella wa Yamoto Band

Msanii wa Bongo Flava, Enock Bella amedai ukimya wake ukilinganisha na wasanii wengine wa Yamoto Band amesababishwa na kutafuta menejiment ila kwa sasa amepata na muda wowote kazi zake zitaanza kusikika.

Akipiga stori na Bongo5  ameeleza pia anashukuru kuona member wenzake wa Yamoto Band wakifanya vizuri  na kazi zao nzuri ambazo zimefika mbali na yote inatokana na wao kuanza kupata menejimenti.

“Kwa sasa nina menejiment mpya ndio tunapanga ratiba ilimradi kazi iende vizuri, ukimya wangu ulikuwa katika michato ya kutafuta menejiment iliyomadhubuti ya kusimamia kazi zangu, kwa hiyo sasa hivi ndio muda mzuri wa kuanza kazi ingawaje ndugu zangu wameanza kwa kuwa wao walianza kupata hizo menejiment,” amesema Bella.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents