Michezo

Huu ndio mwisho wa Ronaldo na Messi katika ulimwengu wa soka ?

Huu ndio mwisho wa Ronaldo na Messi katika ulimwengu wa soka ?

Katika historia ya soka duniani hajawahi kutokea mchezaji aliyewahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani Ballon d or zaidi ya mara tano kama walivyo wachezaji wawili walioandikwa kwenye historia ya soka dunia ambao ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Wachezaji hawa wakizitumikia timu tofauti wamefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani Ballon d’ or kwa nyakati tano tofauti.

Mreno Cristiano Ronaldo alifanikiwa kushinda tuzo ya kwanza akiitumikia klabu ya Manchester United mwaka 2008 baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la UEFA Champions league.

Lakini kwa nyakati nne zote zilizobakia alifanikiwa kushinda tuzo hii akiitumikia klabu ya Real Madrid kuanzia mwaka 2013,2014,2016 na 2017, huku Muargentina Lionel Messi akifanikiwa kushinda tuzo zote akiitumikia klabu yake ya sasa ambayo ni FC Barcelona kuanzia mwaka 2009,2010,2011 na 2012 pamoja na 2015.

Licha ya kushinda tuzo hii mara nyingi zaidi pia wamewahi kushinda tuzo inayotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA ya The best  FIFA men’s player, mbali na tuzo hizo wachezaji hawa wa kihistoria walifanikiwa kushinda tuzo inayotolewa na shirikisho la soka barani Ulaya la UEFA zikijulikana kama UEFA player of the year huku katika tuzo hizo Ronaldo akimpita Messi kwa msimu mmoja kwa yeye ameshinda mara tatu huku Messi akishinda mara mbili. Licha ya kuchuana katika tuzo mbalimbali lakini wachezaji hawa pia wanashindana kimaendeleo pia.

Baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika nchini Urusi mambo yalianza kubadilika kwa wachezaji hawa kwani katika michuano hii wachezaji hawa hawakuweza kuzisaidia timu zao za taifa,Ingawa Ronaldo aliisaidi timu yake ya taifa ya Ureno kushinda taji la Euro mwaka 2016 lililofanyika nchini Ufaransa, lakini katika michuano ya kombe la dunia wote wakiwa hawajawahi kutwaa taji hili licha ya Messi kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kufika fainali ya michuano hiyo mwaka 2014 nchini Brazil ambapo walifungwa na Ujerumani katika fainali goli moja tu.

ZURICH, SWITZERLAND – JANUARY 09: The Best FIFA Men’s Player Award winner Cristiano Ronaldo of Portugal and Real Madrid kisses the trophy during The Best FIFA Football Awards 2016 on January 9, 2017 in Zurich, Switzerland. (Photo by Philipp Schmidli/Getty Images)

Ingawa bado tuzo za Ballon d’or hazijatangazwa mwaka huu,tayari zile tuzo zingine mbili nikimaanisha tuzo inayotolewa na UEFA ikiwa tayari mshindi amepatikana ambapo alifanikiwa kushinda mchezaji kutoka Croatia na klabu ya Real Madrid Luca Modric akiwabwaga Ronaldo na Mmisri Mohamed Salah ambazo zilifanyika Monaco Ufaransa.

Huku tuzo za The best FIFA men’s player of the year zikitangazwa september 24 tuzo ambazo zilifanyika katika Jiji la London nchini Uingereza,mshindi akiwa yule yule Luca Modric akiwabwaga tena Ronaldo na Salah ingawa Salah alifanikiwa kushinda goli la msimu akilifunga katika ligi dhidi ya Everton,na kwa upande wa Ronaldo akitoka mikono mitupu huku Messi nae akiwa hajaambulia kitu.

Swali linakuja katika tuzo za Ballon d’or nani ataibuka mshindi ? je wachezaji hawa walioweka historia kubwa katika soka duniani wataendelea kutawala katika tuzo hizi au ndo basi tena kama ilivyo katika tuzo zile zilizopita ?

Lakini pia wachezaji hawa kwa kuonesha kiwango chao hakirizishi cha kushangaza zaidi wote hawakuweza kuhudhuria wakati wa utolewaji wa tuzo hizi na katika tuzo za UEFA player of the year zilizofanyika Monaco Ronaldo hakuweza kuhudhuria.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents