MichezoUncategorized

Huu ndio ugonjwa unao msumbua Mkwasa mpaka kujiuzulu Ukatibu Mkuu Yanga

Huu ndio ugonjwa unao msumbua Mkwasa mpaka kujiuzulu Ukatibu Mkuu Yanga

Hatimaye Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amefunguka juu ya ugonjwa unao msumbua hadi kupelekea kuchukua hatua ya kujiuzuli kwake ndani ya timu hiyo.

Katibu huyo mwenye historia kubwa na klabu ya Yanga, Mkwasa ameyaeleza hayo kupitia mahojiano yake na kipidi cha michezo cha Esports kinachoruka kupitia radio E FM.

TETESI: Mkwasa ajiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu Yanga

”Mimi nilishaandika barua kwa Mwenyekiti muda mrefu tu kumpa taarifa kwamba kutokana na afya na kutokana na vipimo ambavyo nimefanya nimeshauriwa nipumzike,” amesema Mkwasa

Mkwasa ambaye amepata kuichezea klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ameongeza kuwa ”Na nilikuwa kwa muda mrefu nikifuatilia matibabu familia haikuwa karibu na mimi na mwisho wa siku mara baada ya kumaliza vipimo basi nikaambiwa ni pumzike nisingeweza kuendelea na kazi kwa sababu ni ngumu na inahitaji kuwa fiti.”

”Sasa mimi afya yangu inazidi kuzorota ndiyomaana nikaamua kumuandikia mwenyekiti barua kumjulisha taarifa hiyo kutokana na hali yangu nimeshauriwa kupumzika na hata ripoti ya daktari ninayo mtu akihitaji nitamuonyesha.”

”Kinachonisumbua ni kwenye ‘system’ ya hewa yani kwaamana kwamba kuna matatizo kidogo kwenye mfumo wa hewa kuna matatatizo kidogo kwahiyo nahitaji kupata upasuaji mdogo  ndiyo nipo na familia tunajaribu kuangalia kama tunaweza kupata matibabu.”

”Yanga hawajanijibu na siwezi kusubiri majibu ndiyo ni pumzike, kwasababu ninavyo zidi kuendelea ndivyo ninavyozidi kujiletea matatizo, kwasababu mwisho wa siku nilikuwa napoteza nguvu nashindwa hata kutembea.”

Mkwasa ametangazwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo mnamo Februari 1 mwaka 2017 na kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa muda mrefu iliyokuwa ikikaimiwa na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Tiboroha.

Charles Boniface Mkwasa aliyepata nafasi ya kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa aliwahi pia kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents