Burudani

Huu ndio ujumbe wa mtoto wa Michael Jackson kwenye birthday ya baba yake

By  | 

August 29 kama ya leo ni siku ambayo alizaliwa marehemu Michael Jackson, ambaye alifariki Juni 25 ya mwaka 2009. Mtoto pekee wa kike wa msanii huyo, Paris Jackson hakutaka siku hii muhimu kwa baba yake ipite bila kuandika neno lolote.

Kupitia mtandao wa Instagram, Paris ameandika, “birthday wishes to the love of my life, the one person who showed me what passion truly was, the one that gave me solid morals to live by and how to dream. i will never feel love again the way i did with you.”

“You are always with me and i am always with you. though i am not you, and you are not me, i know with all of my being that we are one. and our souls will never change in that way. thank you for the magic, forever and always,” ameongeza.

Endapo Michael Jackson angekuwa hai mpaka leo angekuwa na umri wa miaka 59 lakini alifariki na kuacha watoto watatu akiwemo Prince Michael ambaye ana umri wa miaka 20, Paris mwenye miaka 19 na mdogo wao wa mwisho Blanket mwenye miaka 15.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments