Habari

Huu ndio ujumbe wa muigizaji kutoka India aliyemuita Iwobi ‘Sokwe’ na baadae kuufuta na kuomba msamaha

Muigizaji wa filamu ya Bollywood, nchini India Esha Gupta ameibua gumzo kali mtandao wa Instagram baada ya kuweka ujumbe unaoshiria mchezaji nyota wa Nigeria na Arsenal, Alex Iwobi ni ‘sokwe’ ambaye uumbaji haujakamilika.

Kwa mujibu wa BBC, Muigizaji huyo alililazimika kufuta ujumbe huo na kuomba msamaha lakini mashabiki wake milioni 3.4 baadhi mashabiki wa klabu ya Arsenal ambayo Alex Iwobi anaichezea walikasirishwa sana na ujumbe huo.

Ujumbe wa Bi. Gupta umeibua gumzo la muda mrefu kuhusu visa vya ubaguzi wa rangi hususan dhidi ya watu wenye asili ya Afrika katika jamii ya wahindi.

“Ujumbe huo haujanishangaza,” Ezeugo Nnamdi aliambia BBC kutoka Delhi, makaazi yake ya miaka mitano.


Muigizaji wa Bollywood Esha Gupta amewahi kuwa muathiriwa wa ubaguzi

Ezeugo ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha wanafunzi wa kiafrika wanaosomea India, alisema kuwa ujumbe wa Bi Gupta ni afadhali ikilinganishwa na visa vya kila siki vya ubaguzi wa rangi wanayokumbana nayo wanafunzi weusi.

“Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida hapa”.

“Wanakuita ‘habshi’ [jina la kudhalilisha], na maneno mengine mabaya ya kibaguzi.”Hapa tunachukuliwa kama wala watu.”

Ezeugo alisema, ”Huhitaji kuenda mabali kuthibitisha hilo, fuatilia kwa makini sinema za kihindi utajionea jinsi wahusika wausi wanavyodhalilishwa katika filamu zao.”

Mwaka 2016 mwanamke raia wa Tanzania alishambuliwa na kuvuliwa nguo na genge la vijana wa kihindi baada ya kuhoji kwanini anabaguliwa.

Kisa hicho kilimfanya mpiga picha Mahesh Shantaram, kutathmini upya hali ya maisha ya watu wenye asili ya kiafrika nchini mwake.

Shantaram, alisikitishwa na kile alichoshudia baada ya kufanya uchunguzi wa miezi kadhaa katika jiji analoishi na maeneo mengine nchini.

“Nilisikia visa vya kiajabu kwa mara ya kwanza,” alisema. “mtu anakusimulia hadithi kuhusu nchi yako ambayo unafikiri unaijua vyema, lakini unafahamishwa hali tofauti.”

Katika visa vingine aligundua kuwa, mtu kuwa na ngozi nyeusi moja kwamoja ni “mhalifu” machoni pa jirani zake.

Matokeo yake? Waafirka wasiokuwa na hatia kama Edurance Amalawa aliishia kushambuliwa na alipoingia duka moja la jumla mjini Delhi mwezi machi mwaka 2017.


Endurance Amalawa alishambuliwa mwaka 2017

Shambulio dhidi ya Amalawa lilitokana na kifo cha msichana wa kihindi aliyefariki baada ya kutumia dawa ya kulevya kupita kiasi.

Wakati huo ilidaiwa kuwa kifo chake kilisababishwa na mlanguzi wa dawa za kulevya kutoka”Nigeria”

Lakini sio watu weusi pekee wanaojipata katika hali hiyo nchini India. Wahindi weusi pia wanakabiliwa na visa vya ubaguzi wa rangi.

Esha Gupta mwenyewe ni muathiriwa wa ubaguzi wa rangi.

Aliwahi kusimulia masaibu yake katika gazeti la Times la India mwaka 2017.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents