Michezo

Huu ndio usajili uliofanyika siku ya mwisho barani ulaya kwa vilabu mbalimbali

Vilabu mbalimbali vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kuimarisha vikosi vyao katika siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi.

Hawa ni baadhi ya wachezaji walio kamilisha usajili.

COBHAM, ENGLAND - AUGUST 31:  David Luiz is unveiled as Chelsea's new signing at Chelsea Training Ground on August 31, 2016 in Cobham, England.  (Photo by Chelsea Football Club/Chelsea FC via Getty Images)

Klabu ya Chelsea imetangaza rasmi beki David Luiz amejiunga tena na klabu hiyo akitokea Psg kwa ada iliyoripotiwa kuwa ni pauni milioni 32.

37C7E5B700000578-3767978-image-a-2_1472711388473

Kiungo Mfaransa Moussa Sissoko ameondoka Newcastle na kujiunga na Spurs kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya pauni milioni 30.

37C5247600000578-0-image-a-1_1472677847317

Klabu ya Bournemouth imetangaza rasmi kumsajili kiungo Jack Wilshere,24, kutoka Arsenal kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu hiyo ni baada ya Arsenal kuzipiga chini ofa za Juventus na Roma.

37C22D2200000578-3767088-Chelsea_have_sealed_a_23million_deal_for_Fiorentina_defender_Mar-a-18_1472661331512

Klabu ya Chelsea imetangaza rasmi kumsajili beki wa kushoto Mhispania Marcos Alonso kutokea Fiorentina kwa ada ya pauni milioni 23.

b9338bad-0897-4121-81af-aeeefe76531c

Kiungo mkongwe kutoka Uholanzi, Nigel De Jong ametua Galatasaray ya Uturuki kwa mkataba wa miaka miwili.

1-26

Stoke City imetangaza kumsajili mshambualiaji Wilfred Bony,27, kutokea Man City kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu.

37C213E400000578-3766785-image-a-2_1472660039493
Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City

37C2694400000578-3766623-image-a-2_1472664037421

Klabu ya Juventus wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Italia imelipa pauni million 4 kwa msimu na kama watamhitaji kabisa, watalazimika kulipa pauni million 8.4.

NORWICH, ENGLAND - APRIL 16: Dieumerci Mbokani of Norwich City signs autographs prior to the Barclays Premier League match between Norwich City and Sunderland at Carrow Road on April 16, 2016 in Norwich, England.  (Photo by Mike Hewitt/Getty Images)

Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City kwa mkopo wa muda mrefu kutoka Dynamo Kiev.

CrMOd29W8AAczWM.jpg-large

Manchester City wamempeleka Samir Nasri kwa mkopo wa msimu mzima katika klabu ya Sevilla.

CrNVhuTXYAAzO8G
Mchezaji Christopher Samba, ambaye ni beki mwenye asili ya Congo. Amejiunga na Panathianakos ya Ugiriki.

7fceba44-0a71-4b6e-9dd7-203cf8b14378

Beki wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa amejiunga na klabu ya West Ham United inayoshiriki Ligi Kuu England, Ingawa dau alilo sajiliwa halijawekwa wazi.

1-30

Kaka wa mchezaji ghali kwasasa Duaniani Paul Pogba, Mathias Pogba ambaye ana pacha wake Patrick amesajiliwa na klabu ya Sparta Rotterdam ya Uholanzi kwa mkataba wa mwaka mmoja, pakiwa na kipengelea cha kuongeza mkataba endapo mchezaji huyo ataonesha kiwango kitakachoridhisha timu hiyo.

37C5228300000578-3766855-Liverpool_striker_Mario_Balotelli_right_has_joined_French_club_N-m-4_1472675515451

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Mario Balotelli amejiunga na klabu ya Nice ya Ufaransa akiwa mchezaji huru.

diego lopez_630x357

Golikipa wa zamani wa Real Madrid, Diego Lopez ambaye sasa ni mchezaji wa AC Milan, amejiunga na Espanyol ya Hispania kwa mkopo hadi Juni, 2017.

37C52D8400000578-3766601-image-a-39_1472678861631

Mabingwa wa Uingereza Leicester City wamevunja rekodi yao ya usajili baada ya kutangaza kumsajili mshambuliaji wa Algeria Islam Slimani,28, kutokea Sporting Lisbon kwa ada ya inayoripotiwa kuwa ni pauni milioni 29, amesaini mkataba wa miaka mitano

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents