Uncategorized

Huu ndiyo mji uliyo na masikini wengi nchini Marekani, asilimia 62.4 ya wakazi wake huishi chini ya dola moja kwa siku

Wakaazi wa mji wa Escobares uliopo katika mpaka wa Mexico na Marekani haukuwahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani.

62.4% ya watu wa Escobares, katika jimbo la Texas ni masikini

Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

“Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu,” anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani.

Débora Hernández,mkaazi wa Escobares.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bi. Debora hajui kusoma na kuandika, anasema alijifungua watoto saba lakini ni mmoja kati yao aliyebakie wengine wote wamefariki.

Alipoulizwa nini kilichosababisha vifo vyao alisema “Sijui, na wala sikuambiwa kilichowasibu”.

Alipokuwa mdogo alipelekwa katika shule ya wanafunzi wanaohitaji huduma maalum. Japo alikamilisha masomo ya msingi hakujifunza lolote.

Licha ya hayo yote Debora amekuwa akiishi na mume wake ambaye hana kazi kwa miaka mitatu sasa.

98% ya wakaazi wa ni watu wenye asili ya Uhispania.

Paa la nyumba yao linavuja kukinyesha na hali yao ya maisha kwa jumla inamfanya mtu kujiuliza ikiwa siku moja mambo yatabadilika.

“Inabidi utoke hapa kila siku kutafuta kibarua vinginevyo utalala njaa”

Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.

“Wale waliyo na stakabadhi zinazohitajika, wanafanya kazi katika eneo la kaskazini,” anasema Homero Rosales.

Homero Rosales

“Cha kusikitisha ni kuwa lazima utengane na familia yako kwa miezi kadhaakwenda kutafuta ajira la sivyo wapendwa wako watakufa kwa njaa.”

Homero ambaye ni baba wa watoto wanne anafanya kazi ya kujenga mabomba ya mafuta katika mji wa Pecos uliyopo Texas magharibi.

“Mwanangu mkubwa alilazimika kuacha shule ili kufanya kazi na mimi”.

Ramani ya Escobares

Wale ambao hawafanyi kazi ya ujezi wa mabomba ya mafuta wanafanya vibarua katika miji mingine au wanategea msaada wa serikali kwa jamii kununua chakula.

“Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,”Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC.

Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa.

12.3% ya watu nchini Marekani ni masikini hii inamaanisha takriban watu milioni 40 hawana uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya msingi

Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya “Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,”anasema mtafiti, Rakesh Kochhar.

Miaka 13 iliyopita mji wa Escobares haukuwepo lakini mwaka 2005 ulitambuliwa kuwa moja ya miji nchini Marekani, kabla ya hapo watu waliyoishi sehemu hiyo hawakua chini ya mamlaka yoyote ya mji.

Baada ya Marekani kusikia kuwa mji wa karibu unaofahamika kama Rome ulikuwa na mpango wa kunyakuwa sehemu ya mji wa Escobares mambo yalibadilika.

Nyunmba za trela ni maarufu sana mjini Escobares

98% ya watu wanaoishi Escobares wanatokea taifa jirani Mexico

Baadhi yao walizaliwa mjini humo na wengine wamepewa urai wa Marekani lakini kuna wale ambao hawana “stakabdhi rasmi” waliyotoroka mauaji na utekaji nyara katika jimbo la Tamaulipas.Ukiwa mgeni katika mji wa Escobares ni vigumu kubaini kuwa ni moja ya miji masikini nchini Marekani.

Hakuna visa vya watu kuishi mitaani kama vile vinavyoshuhudiwa mjini Los Angeles, au kukutana na watu wanaoishi katika hali ngumu kutokana na ubaguzi wa rangi katika miji ya Detroit na Baltimore.

Lakini watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents