Habari

Huu ni kama usumbufu na ubabe – Mhe. Mbowe

Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amefunguka na kusema huu ni kama usumbufu na ubabe kwa namna moja au nyingine, huku kisema Jeshi la polisi walikuwa na uwezo wa kutoa taarifa kwa Mhe. Edward Lowassa asiende leo katika Mahojiano.

Mhe. Mbowe ameyaanisha hayo kupitia Tweet zake alizoziweka kupitia ukurasa wake wa Tweeter huku akisema Polisi walimuita Lowassa arudi tena Polisi leo Juni 29/2017, leo wamemwambia arudi tena Julai 13/2017.

Polisi walimuita Mhe. @edwardlowassatz arudi tena Polisi leo Juni 29/2017, leo wamemwambia arudi tena Julai 13/2017.

Huu ni kama usumbufu na ubabe kwa namna moja au nyingine, walikuwa na uwezo wa kutoa taarifa kwa Mhe. @edwardlowassatz asiende leo.

Waandishi wa Habari wanafukuzwa, unapomuita Kiongozi wa kisiasa kama Mhe. @edwardlowassatz ni habari wanayo haki ya kujua kinachoendelea

Pia wananchi wa haki ya kupata taarifa ndio kazi kubwa ya Waandishi wa Habari kutoa taarifa juu ya masuala mbalimbali yanayojiri.

Kwa Upinzani Waandishi wa Habari kukusanya habari inaonekana ni haramu, hao Polisi kukiwa na taarifa ya kutoa kwa wananchi wanawaita
Inabidi tuongee na Waandishi wa Habari vichochoroni kama iliyotokea pale Makao Makuu ya Polisi.

Polisi wasijaribu kutufunga midomo ni kweli kuna Mashehe wapo mahabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa mahabusu bila kupelekwa Mahakamani
Hatuungi mkono uhalifu ukifanywa na Kiongozi awe wa Kikristo au Kiislam, “Justice delayed is justice denied”

Sisi kama Chama tunalaani mauaji yanayoendelea katika mkoa wa Pwani, msimamo wa Chama ni tunalaani mauaji kwa nguvu zote.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents