BurudaniUncategorized

Huu ni muda wa ‘Bongo Los’, nimeliandaa na limeiva – P Funk

Moja kati ya label kongwe za muziki nchini, Bongo Record ya producer P Funk Majani, imeweka wazi ujio wa kundi lake jipya  ‘Bongo Los’ ambalo hivi karibuni litaachia project mpya.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Mkurugenzi wa label hiyo, P Funk Majani amesema kundi hilo limeundwa na wasanii wawili ambao wote ni rapa.

“Kundi linaitwa ‘Bongo Los’ ni kundi ambalo limeandaliwa kwa muda mrefu, mtarajie muziki mzuri, muziki ambao watu wamechukua muda kuuandaa, muziki ambao umekamilika, muziki ambao utaburudisha watu wengi, muziki wa hisia, vipaji vipya, muziki ambao unajenga. Bongo Los linaundwa na wasanii wawili, kuna binti anaitwa Tammy na msanii wa kiume anaitwa True, na wote ni wasanii wa kufoka, lakini kwenye hii project mpya kuna muimbaji anaitwa Asteria Mvungi, amefanya mambo fulani hivi makali,” alisema Majani.

Aliongeza, “Wakati ujao watashirikiana na wasanii tofauti tofauti ili kupata ladha mpya. Kwahiyo hii project mpya ni kubwa na yakwanza kwao. Video ya ya project yao itatoka weekend hii, pia kuna video nyingi na nyimbo zinakuja. Sisi tunachoomba ni kupata support kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wetu, wasanii, vyombo vya habari pamoja na mashabiki,”

Label ya Bongo Record imewatoa wasanii wengi wakubwa akiwemo Juma Nature, Professor J, Jay Moe, Wateule na wengine wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents