Habari

Huu ni ukweli tunaousahau haraka sana kwenye maisha

Inashangaza pale ambapo tunapoteza mwelekeo katika vitu vya muhimu kwenye maisha yetu. Hii ni kutokana na kazi nyingi na majukumu ya kila siku ambayo yanajirudia rudia. Hebu tuangalie ukweli ambao tunausahau haraka sana kwenye maisha na kazi zetu za kila siku.

woman-thinking

1. Unapokuwa busy sana haina uhusiano na uzalishaji  wake

Hebu fuatilia kila mtu anayekuzunguka. Wanaonekana wana shughuli nyingi sana, kuhudhuria kutoka kikao kimoja kwenda kingine, wanatuma barua pepe n.k. Je kwa ukweli ni wangapi wanazalisha kitu gani? Mafanikio hayaji kutokana na shughuli nyingi au mizunguko mingi, inatokana na kuwa na dira kuhakikisha kwamba muda unatumika vizuri katika kuzalisha kitu au bidhaa husika katika kazi yako au biashara yako.

Unatakiwa kujua wote tuna masaa yale yale lakini uzalishaji umetofautiana kutokana na namna tunavyotumia muda wetu. Wewe ni matokeo uzalishaji wako na si juhudi. Hivyo weka juhudi kwenye jambo ambalo litaleta matokeo bora.

2. Kufanikiwa sana kunatokana na kupitia kushindwa kwingi

Hautaweza kupata ladha ya mafanikio mpaka umejifunza kutokana na makosa. Makosa yako yanatengeneza njia ya wewe kufanikiwa pale yanapovumbua ulipita au haukufanya kwa njia sahihi. uvumbuzi mkubwa huwa unatokea pale ambapo mambo yanaonekana yameshindikana na unaona huwezi kusogea ndipo unaweza kufikiri tofauti na mwanzo na utaweza kujua ni wapi umekosea ili ufanye mabadiliko.

Kufanikiwa kunahitaji uvumilivu na uwezo wa kuwa na tabia au hulka njema wakati unapambana kufikia kule unakotaka kufika katika mafanikio.

3. Uoga ni kitu cha kwanza unaweza kujutia

Ilishasemwa na ni kweli kwamba ukipoteza nafasi pekee uliyokua nayo kufanikisha jambo fulani utagundua kwamba hukuchukua hatua kwa sababu ya uoga wako. Ukiogopa kufanya jambo fulani kwa sababu unaogopa kushindwa, je ukishindwa litakuua? ingawa kifo ndio kitu pekee kinachoweza kuzuia mafanikio yako kufika kule unakotaka, jambo baya sana kutokea kwako ni kuruhusu kufa na kitu moyoni wakati bado unaishi.

4. Uthamani wako lazima toke ndani yako mwenyewe

Pale ambapo hali ya kufanikiwa na kutosheka inatokana na kujifananisha na mtu mwingine, wewe hauna mwelekeo wa maisha yako mwenyewe. Kama unaamini umefanya vizuri na inaonekana umefanya vizuri basi usiruhusu mawazo ya mtu mwingine yakukatishe tamaa endapo anakejeli na kuona si kitu kile ambacho umeweza kukifanya. Linda fikra na mawazo ya mazuri dhidi ya mawazo mabaya kwani ukishindwa kujithamini wewe hakuna mwingine atakayekusaidia kutoka hapo ulipo. Ukiweza kujithamini ni rahisi sana watu wengine kukuthamini na kujua mchango wako katika maisha yako mwenyewe na ya watu wanaokuzunguka.

5. Kiwango chako kinatakiwa kuwa kizuri kulingana na watu wanaokuzunguka

Unatakiwa kuzingirwa na watu ambao wana mwelekeo wa kukufikisha sehemu bora na nzuri. Kama ni watu wanaokurudisha nyuma, achana nao kabisa na wala usiwape nafasi katika maisha yako. Kwanini unatakiwa kuzungukwa na watu sahihi? Unatakaiwa kuwa na watu wanaokufanya uone wewe ni mtu wa thamani na wao wanajisikia kuonekana wa thamani kama wako na wewe. Heshima yako na watu wanaokuzunguka havitakiwi kutofautiana, ukishindwa kufanya hivyo matokeo yake yataonekana tu, hakutakuwa na kuongezeka katika viwango vyako.

6. Maisha ni mafupi sana

Hakuna anayejua kuhusu kesho isipokuwa mwenyezi Mungu. Pale ambapo watu wanakufa haraka wakati walikuwa wanahitajika inatupa muda wa kufikiri tunafanya nini? Je ni jambo gani la muhimu, je tunatumiaje muda wetu? Na je tunaishi vipi na kuwachukulia vipi wenzetu? Kila asubuhi unapaswa kujikumbusha kuwa umepewa nafasi nyingine ya kuishi unaitumiaje? Siku nzuri huanza na fikra nzuri.

7. Huhitaji kuombwa msamaha ili usamehe

Maisha huenda vizuri na rahisi pale ambapo unaruhusu  kinyongo/uchungu na visasi vikuondoke kwa kusamehe hata kama hujaombwa msamaha. Uchungu/kinyongo huchukulia matukio yote ya zamani na kuendelea kuyabeba huku yakikukosesha furaha ya leo. Chuki na hasira ni vitu vya hisia ambavyo vinanyonya na kuharibu furaha ya maisha. uchungu/ Kinyongo kutokana na utafiti ni moja ya vitu ambavyo vinasababisha mtu kuwa na magonjwa ya moyo na msongo wa mawazo.

8. Unaishi maisha uliyotengeneza mwenyewe

Wewe ni matokeo ya maamuzi yako mwenyewe na wala si vitu vilivyotokea kwenye maisha yako. Unaamini hivyo kwasababu ya kile ambacho umeamua kukiaamini. Mazingira mengi tunatengeneza wenyewe, ni sawasawa maisha ya baadaye yanategemea tunafanya nini sasa. Ukijiona umekwama kwa namna moja ama nyingine ni kwasababu hujaweza kuchukua maamuzi fulani juu ya maisha yako mwenyewe, umeruhusu mazingira na watu wanaokuzunguka waamue juu yako.

9. Ishi kutokana na nyakati ulizopo

Huwezi kufikia malengo yako ya maisha kama hujajifunza kuishi maisha ya sasa. Hakuna majuto yoyote unayoweza kuyafanya yakabadilisha kile ambacho umekifanya jana, wala hakuna mtu anayeweza kubadilisha hilo. Ni ngumu kufurahi kama akili ipo sehemu nyingine na mwili upo sehemu nyingine, saidia akili yako na fikra zake ziiishi kulingana na sasa. Hivyo kubali yaliyopita na ujue mambo ya kesho hayajulikani, woga ni jawabu la kulipa deni usilodaiwa.

10. Mabadiliko ni azima inabidi uyakubali tu

Pale ambapo unakubali mabadiliko ndipo unaweza kujua na kutafuta mazuri yake. Unahitaji fikra pana na iliyopevuka ili uweze kujua umuhimu wa mabadiliko. Wakati mwingine tunashindwa kwenye maisha kwasababu ya kutojua mabadiliko ni nini na ni ya lazima. Zaidi ya yote wendawazimu ni kufanya kitu kile kile kila wakati na kila siku huku ukitegemea matokeo tofauti. Maisha hayajasimama na hayamsubiri mtu, kama mambo yanaenda vizuri shukuru na ufurahie na kama bado unatafuta vitu zaidi na unafikiri ndivyo vitakupa furaha inawezekana usiwe hai kukutana navyo uweze kuvifurahia.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents