Michezo

Huu ni utabiri wa Thierry Henry kwa Arsenal

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha SKY Sport, amesema anaamini kwa kipindi hiki kilichobaki kwenye dirisha la usajili, ni lazima Arsenal isajili striker na midfielder.

2BA2D33000000578-0-Thierry_Henry_wants_Arsenal_to_sign_a_defensive_midfielder_or_a_-a-69_1440455785644

Alisema hayo jana wakati wa mechi kati Arsenal na Liverpool iliyochezwa katika uwanja wa Emirate na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

“Nadhani itakua ni wiki kubwa sana, swali ni kwamba watanunua mchezaji, walikua wanakosa wachezaji sana leo usiku, bado wanahitaji holding midfielder na striker pia. Tulikua tunasema hivi tangu mwanzo wa msimu,” alisema.

Katika mazungumzo hayo Henry alisema pia hakuna jinsi zaidi ya kutumia pesa ili kupata mchezaji anayehitajika kama hayupo kwenye kikosi hicho hivi sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents