Burudani

Huu unaweza kuwa wimbo wa Bongo Flava ambao Diamond anaupenda zaidi!

Diamond Platnumz si shabiki wa muziki wa kihindi peke yake.

Diamond

Hitmaker huyo ni mpenzi wa muziki wa wasanii wengine wa Bongo Flava pia na huenda wimbo ‘Pesa’ wa Mr Blue unaweza ukawa ndio wimbo anaoupenda zaidi.

Kwa mara ya pili sasa, Diamond ameutumia wimbo huo kutuma ujumbe kwa mashabiki wake. Jumanne hii, staa huyo alipost kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram kinachoonesha eneo la nje la mjengo wake ambao yeye huuita ‘state house’.

“Nshatembea kwa miguu kabla ya kuwa Mr Blue, hakuna sista duu wala brother duu aliyenijua, zaidi ya joto mvua na jua na msoto ulionikuza nikakua, labda ghetto na washkaji wanaonijua,” anasikika Blue akiimba kwenye kipande hicho cha video alichopost Diamond alichokiandika maneno ‘kabla ya kuwa Platnumz’.

Hii si mara ya kwanza Diamond amepost video yenye wimbo huo.

Mwishoni mwa mwaka jana alipost video iliyomuonesha akiuimba wimbo huo na kubadili baadhi ya mashairi na kuongeza jina ‘Zari’.

Mashabiki wake wameonesha hamu kubwa ya kuwaona wawili hao waliowahi kuwa maadui wakifanya collabo!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents