Michezo

Huyu ndio mrithi sahihi wa Karius na Mignolet Liverpool ?

Huyu ndio mrithi sahihi wa Karius na Mignolet Liverpool ?

Klabu ya Liverpool kutoka nchini Uingereza iko mbioni kukamilisha usajili wa mlinda mlango nambari moja wa klabu ya AS Roma pamoja na timu ya taifa ya Brazil Alisson Becker kwa uhamisho unaokadiriwa kufikia Euro milioni 66.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga rasmi na klabu ya AS Roma mwaka 2016 akitokea Brazil katika klabu ya Sport Club Internacional.

Liverpool wamekuwa wakiitafuta saini ya mlinda mlango huyu ambaye ni miongoni mwa walinda mlango bora kwa sasa duniani.

Pia wamekosa imani na walinda mlango wake kwa kuonekana kuwa ni sababu ya klabu hiyo kutokufanya vizuri katika baadhi ya michuano hasa michuano ya klabu bingwa barani ulaya UEFA katika mchezo wao wa fainali dhidi ya Real Madrid ambapo mlinda mlango wao Loris Karius aliweza kufungwa magoli ya kizembe na kupelekea Liverpool kupoteza mchezo huo,hivyo wakaamua watafute mbadala wake.

Huku mlinda mlango mwingine raia wa Ubelgiji Simon Mignolet akikosa imani mbele ya kocha wa timu hiyo Mjerumani Jurgen Klopp kwani ameweza kucheza michezo michache mno na nafasi kubwa akipewa Karius ambae pia haaminiki tena katika kikosi hicho.

Alisson Becker amekuwa mlinda mlango wa kuaminika sana katika klabu yake ya AS Roma kwani ameweza kucheza michezo yote ya ligi kuu nchini Italia Serie A pamoja na mashindano mengine kama vile UEFA na mengineyo pia katika timu yake ya taifa ya Brazil ameweza kuaminika sana kwani ndio nambari moja katika kikosi hicho cha bwana Tite.

By Ally Jei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents