Soka saa 24!

Huyu ndio mrithi wa Courtois Chelsea endapo atajiunga na Real Madrid

Huyu ndio mrithi wa Courtois Chelsea endapo atajiunga na Real Madrid

Klabu ya Real Madrid imetuma ombi la kuisaka saini ya mlinda mlango nambari moja wa klabu ya Chelsea Thibaut Courtois kwa ada ya uhamisho wa Paun milioni 31.

Courtois alijiunga na Chelsea mwaka 2011 akitokea Genk lakini Chelsea hawakumtumia bali walimtoa kwa mkopo kwenda Atletico Madrid na mapema 2014 waliamua kumrudisha kipa huyo kutoka Atletico.

Endapo mlinda mlango huyo atajiunga na klabu hiyo kutoka nchini Uhispania, Chelsea itawalazimu wajipange kutafuta mbadala wake na inasemekana wako katika hatua za kusajili mlinda mlango mmoja kati ya Peter Cech 36  kutoka Arsenal au Kasper Schmeichel, 31 kutoka katika klabu ya Leicester City.

Mlinda mlango huyo wa Chelsea na raia Ubelgiji alikaririwa akiongelea suala lake la uhamisho na kusema kuwa bado hajaongea na timu yoyote ila pia alizungumzia suala la winga wa Chelsea na raia wa Ubelgiji Eden Hazard kuhusu tetesi za kujiunga Real Madrid amesema yeye atakapoenda Hazard atamfuata kama atabaki vile vile Hazard hana budi.

Huku hazard nae akiwindwa na klabu hiyo ya Real Madrid kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo aliyejiunga na mabibi kizee wa Turin Juventus.

By Ally jei.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW