Burudani

Huyu ndio producer aliyetayarisha albamu mpya ya Jay Z

Jay Z amekuwa ni rapper anayependa kufanya kazi na watayarishaji wa muziki wenye vipaji kupitia albamu zake 13 zilizopita, je unamfahamu mtayarishaji aliyefanya naye kazi kwenye albamu yake mpya ya 4:44?

Rapper huyo kutoka Brooklyn anadaiwa kufanya kazi na mtayarishaji Ernest Dion Wilson maarufu kama No.I.D katika albamu yake hiyo.

Kwa mujibu wa Chris Black ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu Marekani, kupitia mtandao wake wa Twitter amethibitisha kuwa No.I.D ndio ametayarisha albamu mpya ya Jay.

“New Jay-Z album, 4:44, produced entirely by No I.D,” ameandika Black kwenye mtandao huo.
Albamu hiyo itaanza kupatikana Juni 30 ya mwaka huu kupitia mtandao wa Tidal

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents