Michezo

Huyu ndio shabiki wa Chelsea alishtakiwa kwa kumuonyesha vitendo vya ubaguzi wa rangi , Raheem Sterling

Shabiki wa Chelsea anayejulikana kwa jina la Colin Wing, ameshtakiwa kwa kutumia lugha ya kibaguzi kwa raia muingereza ambaye ni mchezaji wa Manchester City Raheem Sterling.


Shabiki huyo wa Chelsea aliyemuonyesha Raheem Sterling vitendo vya ubaguzi wa rangi umekubali kuwa “ameona aibu na kusikitishwa sana kwa tabia yake hiyo ambapo mchezo huo ulifanyika katika dimba la Stamford Bridge siku ya Jumamosi lakini amekataa kutumia lugha mbaya kwa nyota huyo wa Manchester City.

Colin Wing, mwenye umri wa miaka 60, amegunduliwa kuwa yeye ni shabiki wa Chelsea anadai kuwa Sterling ailimpigia mpira baada ya kutoka kwenye mstari lakini baada ya maonyesho yaliyoenekana kwenye vyombo vya habari vya kijamii, ilionekana sivyo na anastahili hukumu kubwa na inahitajika hatua kuchukuliwa.

Chelsea imemsimamisha Mr Wing kwenda kuhudhuria michezo pamoja na wafuasi wengine watatu “wakisubiri uchunguzi zaidi” katika tukio hili, huku Sterling ameripotiwa kuwa amethibitisha polisi kuwa alionyeshwa vitendo vya unyanyasaji wa kiraia katika uwanja wa Stamford Bridge.

“Nina aibu sana na tabia yangu na ninahisi kuwa mbaya sana,” Mr Wing aliiambia Daily Mail, akiongeza kuwa amepoteza kazi yake na tiketi yake ya msimu huko Chelsea kutokana na tukio hilo. “Lakini sikumwita mweusi ****, nikamwita Manc c ***.

“Nimekuwa shabiki wa Chelsea kwa miaka 50 sasa na, kwa sababu ya mahali nilipoketi, nimechukuliwa kwenye kamera kwa wiki nyingi sasa, Ikiwa nilikuwa na historia ya kusema kitu hiki ningekuwa nimechukuliwa kipindi cha nyuma na sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents