Uncategorized

Huyu ndiye Bilionea anayetaka kuinunua Chelsea, amzidi Abramovich kwa utajiri, anawafanya kazi kutoka nchi 22 duniani

Bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe bado ameendelea kuonyesha kutaka kuinunua klabu ya Chelsea huku nia hiyo ikionekana kugonga mwamba mbele ya mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich kutokana na dau dogo aliloweka mezani.

Britain's richest man Sir Jim Ratcliffe retains an interest in buying Chelsea despite becoming the owner of Team Sky this week

Bilionea wa Kiingereza, Sir Jim Ratcliffe anayetaka kuinunua klabu ya Chelsea

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa, Ratcliffe mwaka jana alitoa ofa kwa miamba hiyo ya Premier League lakini bado dili hilo halijakamilika.

Ratcliffe ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 21 hivi karibuni anatarajiwa kuwa mmiliki wa timu ya baiskeli ya Team Sky kabla ya kuinunua na Chelsea.

Roman Abramovich values the club at £2.1bn, with Ratcliffe's offer last year below that figure
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich 

Hatakama, Abramovich hajachukulia kwa umakini mkubwa dhamira ya bilionea huyo wa Kiingereza, dau analotaka yeye ni pauni bilioni 2.1.

Abramovich amekosekana katika dimba la Stamford Bridge karibia msimu mzima kufuatia wakati mgumu anaopitia kwa sasa wa kunyimwa visa kutokana na mambo ya kimahusiano baina ya Uingereza na Urusi.

Hata hivyo mmiliki anafahamu kuwa na paspoti ya Israeli, huwenda ikamruhusu kutua Uingereza pasipo visa.

Abramovich pia anampango wa kuuboresha uwanja wa Stamford Bridge na kuuongeza uwezo wa kuingiza mashabiki kutoka idadi ya watu 41,631 na kufikia 63,000 ifikapo msimu wa mwaka 2023/24. Hata hivyo kutokana na maboresho ni ishara tosha kuwa Chelsea haiwezi kuuzwa kwa sasa.

Ratcliffe anaifuatilia Chelsea kwa sababu ni karibu na nyumbani kwake anapokaa.

Kwa mujibu wa Sunday Times ya mwaka 2018, ilitoa utofauti wa utajiri wa watu hawa wawili, Ratcliffe anamiliki utajiri wa paundi bilioni 21.05 wakati Abramovich anamiliki utajiri wa pauni bilioni 9.3.

Wakati kampuni yake ya ‘Ineos’ inarekodi ya kuuza pauni bilioni 45 na kuwa na jumla ya wafanyakazi zaidi ya 18,500 kutoka nchi 22.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents