Michezo

Huyu ndiye mchezaji ghali zaidi Everto FC inayodhaminiwa na SportPesa

Imechukua zaidi ya miaka 10 kwa klabu ya Everton FC, kufikia mafanikio ya mchezaji wao Duncan Ferguson raia wa Scotland aliyetokea klabu ya Rangers mwaka 1993 kwa dau lililoweka historia kwa wakati huo ndani ya Everton la uhamisho wa pauni milioni 4.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa yaScotland na klabu ya Everton, Duncan Ferguson 

Ferguson mbaye amefanikiwa kushinda magoli mengi zaidi katika Ligi kuu iliyofikia mpaka kutwaa tuzo ya mchezaji bora.

Mchezaji ghali zaidi kwa sasa ndani ya klabu ya Everton Romelu Menama Lukaku hajaweza kuvunja rekodi iliyowekwa na Ferguson licha yakuwa ndiye anayevuta mkwanja mrefu zaidi ndani ya Blues.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Everton FC, Romelu Menama Lukaku

Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye mkataba wake unamfanya asalie katika viunga vya Goodson Park kwa miaka mitano ijayo anakadiriwa kulipwa pauni milioni 140,000 kwa wiki kiasi ambacho kinaelezwa hakuna mchezaji mwingine yeyote bdabi ya klabu hiyo amewahi kupata.

Baada ya kusajiliwa mwaka 2014 akitokea katika klabu ya Chelsea kwa mkopo alipokea kitita chafedha pauni 28,000,000 ambacho pia kiliweka rekodi ndani ya klabu hiyo.

Lukaku amefanikiwa kuweka rekodi angali akiwa kijana mdogo mwenye umri wamiaka 16 baud ya kuisadia timuyake ya Anderlecht kutwaa ubingwa nichini Ubelgiji.

Mafanikio ya mchezaji huyo hayashangazi wats zaidi kwakuwa ametokea katika familia ya mpira, baba ake mzee Roger Lukaku alikuwa mchezaji ndani ya klabu ya Zaire huku mjomba wake Boli Bolingoli-Mbombo ni mchezaji wa Club Brugge wakati mdogo wake akionekana kufuata nyayo za kaka ake baada ya kujiunga na klabu ya vijana ya Anderlecht’s youth academy.

Msimu wa mwaka 2016/17 Romelu Lukaku ameifunga klabu yake ya Everton FC jumla ya magoli 25, huyo ndiye Romelu Menama Lukaku mchezaji ghali zaidi ndani ya kikosi cha kocha Mholanzi Ronald Koeman aliyeanza kukifundisha kikosi hiko cha Goodson Park toka mwaka 14, 2016

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents