Michezo
Huyu ndiye mfalme wa assist, sio tena Mesut Ozil
Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye anachezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Mesut Ozil alikuwa anatajwa kama ndiye assist King, ikiwa na maana yeye ndio mtaalam wa assist au mkali wa kutoa pasi za mwisho za goli, lakini February 4 mtandao wa sokkaa.com unaripoti kuwa amezidiwa na kuwa nafasi ya pili sawa na Neymar wa klabu ya FC Barcelona nafasi ya kwanza ikiwa imeshikwa na mchezaji Henrikh Mkhitaryan wa Borussia Dortmund.
Henrikh Mkhitaryan ambaye ni mchezaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Armenia saivi ndio unaweza muita assist king kwa bara la Ulaya, ana jumla ya assist 17 na goli 17, hizo ni assist za jumla ya mashindano yote aliyocheza hadi sasa msimu huu.