Burudani

Huyu ndiye msanii wa kike anayetarajiwa kutamba mwaka wa 2017 nchini Kenya

Mwanamuziki na Mshindi wa shindano la Maisha Superstar kutoka nchini Kenya Phillis Ng’etich aka Phy ambaye mwaka 2015 alichuana na wenzake wa na kuwabwaga katika kinyang’anyiro hicho Afrika Mashariki, akiwemo Spirit Soul kutoka Uganda na Damian Soul kutoka Tanzania, anazidi kuonyesha makali yake katika muziki.

Baada ya kushinda shindalo la Maisha superstar, Phy hakutosheka na mafanikio hayo ambayo alitia kibindoni takribani milioni 1.2 zenye thamani ya pesa ya Kenya na recording deal. Phy amekuwa akitumia fursa hiyo kuing’arisha nyota yake ya muziki siku baada ya siku, huku akichia vibao vya muziki vitamu vikiwemo, Ruka alichowashirikisha marapper wakali Kenya King Kaka na Kaligraph Jones na Taboo ambacho kibao hicho ndicho kinamweka juu kwa sasa.

Wakati wanamuziki wengi Afrika Mashariki wanapong’ang’ania nafasi za kupata air play katika vituo vya habari nchini mwao na kwa majirani, Phy alipata bahati ya kuingia kwenye enzi ya wasanii wanotambulika ulimwenguni pale alipojumuishwa kwenye segment ya kituo cha CNN.

Ng’etich alikuwa kati ya wasanii watatu waliowakilisha Afrika Mashariki katika kipindi cha African Voices ambacho kinachoangazia vijana wanaopiga hatua za juu kimaisha barani Afrika na hurushwa na CNN kila wiki ambapo aliwakilisha Kenya huku Tanzania ikiwakilishwa na nguli wa muziki Afrika president wa WCB Baba Tiffa aka Diamond huku nchi ya Senagal ikiwakilishwa na Side Adamo.

Tokea kurushwa hewani kipindi hicho na CNN, Phy amekuwa gumzo Kenya haswa kuwepo kwa Diamond katika segment hiyo hiyo, ambaye anatumika kama kipimo cha masanii wa kimataifa na mwenye ufanisi wa hali ya juu Afrika. Mbali na hivyo, tayari Phy njia zake kimuziki barani Afrila zinatazamiwa kufunguka zaidi mwaka huu wa 2017 ambao tu ndio umeanza na kama walivyonena walumbi siku njema huonekana asubuhi.

Mashabiki wake wanategemea makubwa kutoka kwake, na collabo ya awali aliyoifanya na King Kaka na Kalighraph Jones inahitaji kupigwa jeki na Phy mwenyewe kwa kufuata njia za msanii Diamond ambaye huzitumia fursa kama hizo kujijenga katika himaya ya mziki wake.

Nimekusongezea hapa chini video ya awali ya Phy aki-perform kwenye shindano la Maisha Superstar hapo chini, ilikukumbusha jinsi alivyowapapa na kuwaburudisha mashabiki, majaji na wapenzi wa burudani kote Afrca Mashariki, ambapo pia aliimbuka kuwa mshindi.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : @ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents