Soka saa 24!

Huyu ndiye mwamuzi anaeongoza kwa kadi nyekundu Uingereza, ashatoa 99, wachezaji wahofia huwenda akafikisha ya 100 mechi ya Man City dhidi ya Chelsea

Mike Dean ni jina maarufu ligi kuu nchini Uingereza ambapo kazi yake kubwa ni kupuliza kipyenga awapo katikati ya uwanja na kusimamia sheria 17 za soka huku siku ya Jumapili mwamuzi huyo atakuwa kwenye dimba la Etihad mchezo baina ya Man City dhidi ya Chelsea.

Umaarufu wa mwamuzi, Mike Dean unatokana na kuwa na idadi kubwa ya kadi nyekundu ambazo amezitoa uwanjani kwa wachezaji wasumbufu na wale wanaonekana kuvunja ile kauli ya soka ya ‘fair play’ kiasi kinachompelekea kufikia jumla ya kadi nyekundu 99 ambazo ametoa mpaka sasa ikiwa kama sehemu ya adhabu huku wachambuzi wa soka wakitarajia huwenda akafikisha ya 100 siku ya Jumapili pale kwenye dimba la Etihad.

Mwamuzi huyu alianza rasmi kazi yake ya kusimamia sheria za soka kwwenye Premier League tangu Mwezi Septemba mwaka 2000, alipoisimamia Leicester City ikiwa nyumani dhidi Southampton.

Image result for mike dean

Dean ilimchukua hadi Aprili 14 tu, ndipo kuanza kuonyesha makali yake ya kusimamia sheria baada ya kumtoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji wa Newcastle, Nolberto Solano kufuatia kuunawa mpira kwenye mchezo dhidi ya Ipswich.
Katika umri wake wa miaka 50, inakadiriwa kuwa na wastani wa 4.7 wa kutoa kadi nyekundu kwenye mechiu anazosimamia.

Hizi ni baadhi ya timu ambazo zimeambulia kupata kadi nyingi nyekundu kutoka mwamuzi huyo.

Waamuzi wanaoongoza kwa kutoka kadi nyekundu mpaka sasa, Mike Dean akiwa kinara kati ya hao.

Kusimamia mchezo baina ya Manchester City dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili huwenda kukawatia hofu wachezaji watimu zote mbili hasa wao kuwa vinara wa kupata kadi nyingi nyekundu kutoka mwamuzi, Mike Dean.
Hivyo wachezaji watapaswa kuonyesha tabia njema wawapo uwanjani ili kuepuka kupata kadi nyekundu, ambapo pia itifikisha jumla yake 100 kwakuwa mpaka sasa ameshatoa 99.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW