Uncategorized

Huyu ndiye Paka aliyerithi Tsh Bil 466, aishi maisha ya kifahari, kwa siku anakula aina nne za vyakula, amiliki akaunti za kijami Twitter na Instagram

Taarifa zimeibuka kwamba mbunifu mavazi aliyeaga dunia Karl Lagerfeld amemuachia paka wake sehemu ya utajiri wake wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 200 ambayo ni sawa na bilioni 466 za Kitanzania.

Mbunifu huyo, raia wa Ujerumani, ambaye alikuwa mbunifu mkurugenzi wa kampuni za Chanel na Fendi, alifariki Paris Jumanne akiwa na umri wa miaka 85.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Alimlea paka wake wa dhati na alivutia ufahari aliokuwa nao kwa paka wake anayefahamika kwa jina la Choupette tangu alipokabidhiwa mnamo 2012.

Lagerfeld ameliambia jarida la Ufaransa Numero mwaka jana kwamba amemueka paka huyo kwenye wasia wake kama mmoja wa warithi wa makaazi yake ya kifahari.

Katika mahojiano hayo, alisema Choupette yumo ndani ya urathi, ‘miongoni mwa wengine’. Lakini ameongeza : “Usijali kuna mali ya kumtosha kila mtu.”

Karl Lagerfeld

Lagerfeld akiwa karibu na mchoro wa Choupette

Tayari Choupette ana utajiri wa kiasi, akiwa amejipatia dola za Kimarekani milioni 3 kutokana na matangazo ya biashara kwa kampuni ya magari Ujerumani na kampuni ya vipodozi ya Japan akiwa na mmiliki wake Lagerfeld.

Katika mahojiano tofuati na Numero, Lagerfeld amefichua kwamba amemuajiria paka huyo mayaya wawili, ili kumshughulikia, ambaye amesema anakula “vyakula vinne tofuati” kwa siku anavyotayarishiwa katika ‘mabakuli ya aina yake’.

Alimuezesha Choupette kuwa nyota katika mitandao ya kijamii, akiwa na ukurasa wake katika Twitter na Instagram ambazo zina takriban wafuasi 200,000 kwa pamoja.

Wanyama wanaofugwa kwa fahari na starehe kubwa

Lagerfeld sio tajiri pekee anayetaka kumuachia mnyama anayemfuga mali kushughulikia maslahi yake.

Mbunifu mwingine wa mavazi Alexander McQueen aliacha £50,000 katika urathi wenye thamani ya £16m ili mbwa wake watendekezwe maishani mwao yote.

Oprah Winfrey inaarifiwa ameweka mipango ya kuwacha $ milioni 30 kwa ajili ya kuwashughulikia mbwa wake.

Bubbles the chimpanzee

Sokwe wa Michael Jackson Bubbles alikuwa akivalishwa nguo sare na mmiliki wake

Lakini sokwe kwa jina Bubbles, aliyemilikiwa kwa wakati mmoja na marehemu muimbaji Michael Jackson, hakuwa na bahati sana.

Alipokuwa mkubwa, na kuanza kuonyesha dalili za ukali, aliepelekwa katika hifadhi ya wanyama pori .

Punde baada ya kuhamishwa, Jackson hakulipa tena malipo ya kushughulikia kwake Bubbles.

Wasimamizi wa makaazi ya muimbaji huyo sasa wanatuma kiasi cha pesa katika hifadhihiyo huko Florida kila mwaka, lakini inaarifiwa sio fedha kamili za kumshughulikia sokwe huyo.

Bubbles amelazimika kujikimu atahivyo. Sehemu ya talanta aliye nayo katika sanaa huuzwa kupata pesa za kukimu mahitaji katika hifadhi hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents