Burudani

‘I Miss You’ yamkuna Diamond

Baada ya kuachia video ya wimbo wake wa ‘I Miss You’ ambayo iliwahi kuvuja muda mrefu kidogo, Msanii wa muziki kutoka 255 Diamond Platnum ameonesha kufurahia views wanaoitazama video hiyo mtandaoni.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameonesha wazi wazi furaha hiyo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuitazama video hiyo kwa kuandika “611,054 Views within a Day and few hours….Views Laki sita na kumi ndani ya siku Moja na Masaa….. Eish! Nyie Mafans Mie Nawapenda Ujue jamani?? #IMissYou,”

Hata hivyo ngoma hiyo imezidi kutikisa mtandao wa YouTube kwa kushika video namba moja inayo’trend kwa sasa huku ikiiacha mbali ngoma yake mpya ya ‘Fire’ aliyomshirikisha Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria ambayo nayo ilitoka siku moja na ‘I Miss You’

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents