Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Ibrahim Ajibu atimkia Misri kuanza maisha mpya ya soka

By  | 

Mshambuliaji fundi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Misri kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo awali zilidai kuwa Ajibu ameondoka bila kutoa taarifa kwa uongozi wa klabu, lakini baadaye meneja wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amethibisha kuwa uongozi una taarifa na umetoa baraka kwa mchezaji huyo kwenda kutafuta nje ya Tanzania.

“Ajibu kaenda Misri kwajili ya majaribio na kapata ruksa ya viongozi kama ilivyo ada ya klabu ya Simba, Simba haimzuii mchezaji wake akipata timu ya nje,” Amesema Mgosi.

Ingawa Mgosi amesita kutaja timu ambayo Ajibu anakwenda, lakini taarifa zinaeleza kuwa anakwenda katika timu ya Harass El Hadood.

Source: EATV

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW