Michezo

Ibrahimovic kuendelea kubakia Manchester United

Klabu ya Manchester United imesema itamuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic kulingana maneno ya meneja Jose Mourinho.

3a82c20700000578-3958812-image-a-3_1479766611933

Mchezaji huyo kutoka Sweden mwenye umri wa 35, alitua Old Trafford katika uhamisho wa bure katika msimu huu akiwa na uwezo wa kuongeza mkataba mwingine kwa msimu wa pili. Amesha funga mabao 17 katika mashindano yote msimu huu.

Mourinho alisema: Tutaanda mpango wa kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwemgine .Baadaye anaweza kufanya atakacho.

Ibrahimoviv alisema: Najihisi vyema, nikiwa nitaendelea itakuwa mwaka mwengine.

Ibrahimovic ambaye ameshafunga mabao 62 katika mechi 116 akiichezea Sweden kabla ya kustaafu katika soka ya kimataifa mnamo mwezi Juni, alihama klabu ya PSG mwishoni mwa msimu uliopita

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents