Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Ice Boy atupilia mbali tuhuma za kutoka na mpenzi wa Darassa

Msanii Ice Boy ameeleza kushangazwa na taarifa za yeye kutoka kimapenzi na mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wa rapper Darassa.

 

Ice Boy amesema huyo mrembo ni rafiki yake na wanafanya wote biashara na kila mmoja ana shughuli zake na vitu vingine kuhusu wao ni vya ndani zaidi ila kilichoibua hilo ni baada ya kuweka picha kwenye mtandao wakiwa pamoja.

“Kwa sababu tu nilimposti watu kibao wakachanganya mambo, sasa dili nini?, kwa sababu ni demu wa Darassa. Sio mvutano, sidhani kama ni mvutano kwa sababu mimi sijawahi kuonana naye au kupata comment kutoa kwake hata sijawahi kujua kwamba ni demu wake,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Halafu you never know unaweza kukuta Darassa ameshawahi kudate na mademu kibao ambao wanadate na wana tu halafu yeye mwenye hana hata mchongo nao kwa sababu mademu siwapo tu mshikaji wangu,” amesema Ice Boy.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW