Burudani

Ice Cube atangaza ujio wa ‘Last Friday’

By  | 

Moja ya muasisi wa kundi la muziki la NWA (Nigga With Altitude) Ice Cube kutokea nchini Marekani, ambaye pia ni muigizaji wa filamu kama vile Friday iliyotoka miaka 22 iliyopita, amethibitisha ujio mpya wa filamu hiyo.

Cube amethibitisha kauli iliyotolewa mwezi April tarehe 21 na John Witherspoon, kuwa wanatarajia kuirudisha filamu hiyo tena katika ulimwengu wa sanaa, kauli ambayao aliitoa Katika kipindi cha “The Late Late Show” cha James Corden.

Filamu halisi ya Friday ilitoka mwaka 1995 na pia ikarudia kutolewa upya mwaka 2000 ikiitwa Next Friday, kufika mwaka 2002 ikatoaka tena na kuitwa Friday After Next na sasa itaenda kuitwa Last Friday.

Ice cube amekuwa akishiriki katiaka uigizajia na utaarishaji filamu kama vile Friday, Barbershop, Are We There Yet? na 21 Jump Street. Na kwa mwakani tutegemee kumuona katiaka muendelezo wa filamu ya Ride Along 3.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments